Tuseme ukweli: Misaada ya nje ndio kichocheo cha umasikini Tanzania

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Tanzania ni Nchi Masikini.
Umasikini wa Tanzania kamwe hautaondolewa na Misaada kutoka nje.
Tafiti zinaonyesha zaidi ya 1/4 ya nchi kusini mwa jangwa la sahara ni masikini leo zaidi ya mwaka 1961 japo wanapokea misaada.

Misaada yote hutolewa kwa maslahi ya watoa misaada na sio masikini aliyeko kijijini.
Misaada pekee yenye maana ni ile ya afya ambayo itamfanya mtazania kuwa mzima na kujiendeleza mwenyewe.
kipindi ambapo afrika ilipokea misaada mingi mwaka 1980-1990 ndicho kipindi ilikuwa masikini zaidi

Nchi hii itaendelea kwa Kodi zetu wenyewe wananchi na juhudi za wananchi sio vinginevyo.

Ukiacha misaada ya Kiafya inayotufanya tuwe wazima tukafanye kazi. Duniani kote wazo linaloonekana ni sahihi ni ukweli kwamba Misaada mingine kwa Masikini zinawaumiza badala ya kuwasiadia.Katika harakati zote za kumsaidia masikini duniani hakuna iliyofanikiwa kwa kuwapa misaada, sana sana inawapa nafuu ya taabu zao.

Wakati tunaendelea na mapambano dhidi ya umasikini wetu "Ni Sharti tuukumbatie Ukweli kwamba TANZANIA itaendelea kwa Juhudi za watanzania, na Siku ukiona inapokea misaada michache saana tena kila mwaka zikizidi kupungua."
 
Back
Top Bottom