Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,599
- 6,669
Salaam Wakuu,
Mimi ni mwandishi wa kujitegemea wa habari za uchunguzi.
Mwaka huu nimepanga kutoa mchango katika ujenzi wa nchi yangu kwa kuibua kero na changamoto zinazozikabili Sekta Kuu za Huduma na Ustawi wa Jamii (Maji, Afya, Elimu na Kilimo).
Kero hizo ni zile ambazo hazijaibuliwa na vyombo vya habari au hazijamulikwa kwa kiasi cha kutosha na hivyo kushindwa kusababisha uwajibikaji wa mamlaka husika au kuleta mabadiliko tarajiwa.
Katika awamu yangu ya kwanza nimepanga kuzama katika Sekta nilizotaja kwenye mikoa mitano (5) yaani Dodoma, Tanga, Mwanza, Katavi na Dar es Salaam.
Nina ombi moja kwako mtanzania mwenzangu mzalendo. Kama una taarifa (news tip) yoyote ambayo inakwamisha huduma bora kwenye Sekta ya Maji, Afya, Elimu au inarudisha nyuma ustawi wa Wakulima kwa kudumaza Sekta ya Kilimo, naomba uiwasilishe kwangu ili niweze kuimulika. Watoa dondoo wote nawahakikishia usalama wao na taarifa zao.
Miongoni mwa dondoo nitakazofurahi kupokea nini:
↘Maendeleo ya miradi, urasimu, ufisadi na changamoto ya upatikanaji wa maji ya uhakika kwenye mikoa ya Dodoma, Tanga, Mwanza, Katavi na Dar es Salaam.
↘Ufanisi wa usambazaji wa madawa na vifaa tiba, upatikanaji wa madaktari na wasaidizi wao katika mahospitali, zahanati na vituo vya afya. Upatikanaji wa vipimo na ubora wa vipimo vya maabara kwenye mahospitali, n.k kwenye mikoa ya Dodoma, Tanga, Mwanza, Katavi na Dar es Salaam.
↘Uwiano kati ya idadi ya walimu na wanafunzi, sababu za wanafunzi kutofanya vizuri katika masomo, upatikanaji wa vifaa vya kufundishia mashuleni, vyuo feki, vyuo vinavyotoa kozi ambazo hazijasajiliwa, utapeli wa wahasibu vyuoni, ukosefu wa maadili kwa wanachuo na wahadhiri, ufisadi katika miradi ya vyuo vya umma, ubadhirifu katika mifuko ya elimu hususani katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Mwanza, Katavi na Dar es Salaam.
↘Ufanisi na ubadhirifu katika usambazaji wa pembejeo za kilimo, mtandao wa dawa na mbegu feki, unyonyaji na manyanyaso ya wakulima, changamoto ya huduma za ugani, uduni wa vyuo vya utafiti wa masuala ya kilimo na mifugo, migogoro ya mashamba, n.k vyote kutoka katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Mwanza, Katavi na Dar es Salaam.
Mawasiliano:
Dondoo zote zitumwe kwenda baruapepe ifuatayo:
jielezehuru@gmail.com