Eng. Y. Bihagaze
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 1,487
- 913
Wadau Wenzangu
kadiri Siku zinavyo kwenda kwa kasi, Nyakati za uchaguzi mkuu wa madiwani, Wabunge na mkuu wa kiti unasogea zaidi, Ni vema tukawekana sawa mtu asijesema hakuambiwa yakamkuta ya kumkuta.
kasi hii ya kusogelea uchaguzi inakwenda sambamba na kasi ya shauku ya wengi, vijana kwa wazee kutamani position fulani ya kisiasa. Nia na shauku hii ilikuwepo muda mrefu but as days aproach to the point shauku na matamanio haya imezidisha mori na mihemko kiasi kwamba vituko na vimbwanga vingi vimeanza na vitazidi kujitokeza. Watu wanazidi kuchanganyikiwa wanapowazia kuwemo mjengoni, wanapowazia kuwa kina Halima Mdee au kina Kafulila, mtu anapowazia kumiliki kitu kama VX.. hii inamchanganya kiasi cha kuchukua maamuzi "magumu yanayo weza kumcost baadae'. Maamuzi Yoyote ambayo nyuma yake kuna msukumo mkali lazima uyapime na kuyatafakari kwa kina.
mtu ingawa hana Title yoyote, ingawa pia hajawahi fanya chochote cha maendeleo zaidi ya kumiliki shahada au stashahada yake ya elimu, anajifariji kwa mtaji wa elimu atalichukua Jimbo zima. akili hii maskini inamsukuma kuacha kazi!!! anaacha kibarua chake, akili yake ameshaituma jimboni kwamba kwa mtaji wa elimu yake na mambo mawili matatu atalichukua jimbo. kuna akili nyingine mbaya zaidi anayoweza kiuwaza kwamba akikosa ubunge kwa sababu ana elimu atasaka ajira upya, ataipata, atarejea kwenye maisha ya mshahara. I hate this..
Tuwekane wazi na kuonyana mapema, USIACHE KAZI KUUFUKUZIA UBUNGE/UDIWANI AU URAISI. Kwa sababu hata hiyo kazi unayo fanya ni sehemu ya Uraisi, Ubunge au Udiwani. kama Ukiwa bado Kijana,Ukaamua kuacha Ajira yako, na kujitosa Jimboni, tunakukaribisha kwa mikono Yote, wewe ni mzalendo na mwanajimbo. Acha mawazo ya ki-abunuasi, unaweza kuteuliwa kugombea nafasi ya kisiasa au jina lako likakatwa, unaweza kupita ukagombea nafasi ya kisasa ukashindwa vilevile kwenye uchaguzi, au unaweza ukashinda ukanyang'anywa ushindi mchana kweupe, ukatumia maisha yako kukimbizana na mahakama on that time na kazi huna utakula nini na familia yako.
NJOO jimboni, igeuze akili yako na elimu yako ifae jamii, Tumia akili, Ujuzi, na elimu yako kuleta maendeleo kwa jamii. buni Miradi, anzisha vikundi, buni shughuli za maendeleo, fanya vitu vionekane kiasi jamii inufaike na Kipaji au elimu yako. Elimu, Ubunifu, Moyo, Nia na Bidii yako hatakama itaanza kwa kusuasua hatimae itashamiri na kuzaa matunda yatakayo ifaa jamii ndogo inayo kuzunguka, kijiji, jimbo, wilaya hadi Taifa kwa ujumla. jiamini kwamba mwenyezi Mungu ameweka kitu ndani yako lazima kikue, huo ndio ubunge na uwakilishi wa maana zaidi ya kukimbilia huko mjengoni.