Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,800
- 34,189
"Uke bora ni Fahari ya Mwanamke na Furaha ya Mumewe"
Uke bora hautoi harufu mbaya, hauna fangasi si mgumu wala mlaini, una majimaji kiasi na pia una uchumvichumvi ulio wa kawaida.
Uke bora ni fahari ya mwanamke na furaha ya mwanaume. Uke bora utakufanya mwanamke ujithamini na kujiamini.
Kuna mambo ambayo yanaweza kuharibu uke wako na hatimaye kutowesha fahari yako na furaha ya mumeo. NOTE: Uke kwa kawaida hujisafisha wenyewe kwa ndani lakini kutokana na ulaji hovyo wa chakula, uingizaji wa vitu vingeni ukeni na upakaji wa mafuta ya ajabu uumeni hivyo kuweka uwiano wa asidi na tindikali ndani ya uke kuwa sio mzuri hivyo uke unashindwa kujisafisha na kuuwa wadudu.
WAJUE MAADUI 10 WA UKE WAKO
1.KUINGIZWA AU KUJIINGIZA VIDOLE/NA VITU VIGENI UKENI BILA KUNAWA MIKONO YAKO VIZURI.
Kabla ya tendo la ndoa ni kawaida kuingiza vidole sehemu ya uke ili kuamsha amsha hamu na kujiweka sawa kwa ajili ya shuhuli.
Hilo sio tattizo, tatizo linakuja pale ambapo hujanawa mikono yako vizuri na hivyo kuingiza wadudu mbalimbali uliowakusanya katika shughuli mbalimbali wakati wa mihangaiko yako ya kila siku.
Pia wengine hutumia vitu mbalimbali vingine vina ncha kama matango, ndizi, midoli na vinginevyo
NI VIZURI KUNAWA MIKONO YAKO VIZURI NA PIA SAFISHA VIZURI HIVYO VIFAA UVITUMIAVYO KUINGIZA AU KUJIINGIZA UKO UKENI
2. KUDO- KINYUME NA MAUMBILE
Kwenye haja kubwa kuna idadi kubwa ya wadudu wa magonjwa kuliko sehemu yeyote chafu unaijua. Sasa kama unatumia pande hizo basi tambua ya kwamba unaeneza magonjwa yatakayosababisha uke uwe na afya legelege
3. KUKAZA UKE
Wanawake wengi wanatumia mbinu mbalimbali ili kuufanya uke uliolegea uwe 'tight' wengi wanatumia dawa zenye kemikali. Matokeo yake uke umekuwa kama uwanja wa mpira na wengine wameutaitisha mpaka unakuwa kama wa mtoto na hivyo kuhitaji tena kwenda kwa madaktari
4. ADHABU KWA WASICHANA WA KAZI, WATOTO WA KIKE NA WAMAMA WAZIMA
Kuna adhabu zinazoathiri uke moja kwa moja, umesikia wanawake wasipigwe viboko matakoni, lakini huko majumbani watu wanapigwa hadi ukeni mpaka basi, wengine wanawekewa pilipili na tangawizi sehemu za siri, wengine wanaingizwa vitu za ajabu ajabu.
5. UNAPOKOJOA UMECHUCHUMAA
Wamasai wanakojoa wamesimama na wanachekwa sana, but they have a point to tell. Mwanamke unapoenda choo ya jumuia, mfano kazini au chuoni au shuleni, huna uhakika na usafi uliofanywa na yule aliyetumia choo kabla yako. Pia hujui ana magonjwa gani. Sasa unapokojoa au kujisaidia huku umechuchumaa au kukalia kingo za tray za choo ni rahisi sana uchafu kukurukia na kukuingia, utapata magonjwa ya ngozi UTI na mauvimbe ya ajabu ajabu.HAKIKISHA USAFI WA UNAPOJISAIDIA
6. USAFI WA NGUO ZA NDANI
Tumia nguo yako ya ndani mara 1 kwa siku kama inawezekana badili mara 2. Hakikisha nguo ya ndani unayotumia ukiwa period haitumiki wakati unapokuwa hauko period. Pia tumia sabuni zinazouwa wadudu wakati wa kuosha nguo zako za ndani hasa za wakati upo period, ili ule uchafu uliobakia kwenye nguo za ndani kwa kuwa hukuosha vizuri chupi wakati uko period usije unda wadudu waharibifu na kuingia ukeni siku NI VZR KUWA NA NGUO ZA NDANI ZA KUTOSHA NA KUCHAGUA ZA KUVAA UKIWA PERIOD
7. TUMIA PEDI SAHIHI
Tumia pedi zenye pamba laini, zenye kuingiza na kutoa hewa vizuri, pedi zinazotengeneza oxygeni, pedi za thamani ya uke wako, pedi zinazoweza kukukinga na magonywa, pedi ambayo hata ukiwa swimming pool haiwezi ingiza wadudu wala chlorine ukeni. Tumia pedi zilizoundwa kwa ajili ya uke siku za kawaida na siku za hedhi. Badilisha pedi mara kwa mara katikati ya siku na tumia pedi bora wakati wa usiku. Kama una pesa usije ukabania mahitaji ya uke, utunze kwa gharama yeyote BILA KUUATHIRI
8. JITIBU MAGONJWA
Magonjwa kama UTI, hedhi mvurugiko, Bawasiri na upele wa ajabu sehemu za siri vinaharibu afya ya uke wako. Hakikisha unatibu magonjwa hayo mara moja na sio kukaa muda mrefu na maradhi
9. KULA NA KULALA HOVYO.
Hakikisha unalala si chini ya masaa8 kwa siku. Ulaji hovyo wa chakula umekuwa ndio kisa namba 1 cha magonjwa mengi na mapya duniani kote. Mwanamke unakula nyama na pombe, chips na wali haujali afya yako hata kiduchu. Uke nao unahitaji lishe bora kwa ajili ya usafirishaji wa damu, viinilishe na madini mbalimbali hadi sehemu za ukeni. Hii ni muhimu kwa ajili ya kuweka uke imara na tayari kwa kutimiza majukumu mbalimbali kama uzazi na pia tendo la ndoa. Ulaji wa vyakula visivyo rafiki unasababisha baiologia na kemia asili ya uke kubadilika na hivyo kuleteleza magonjwa na tabia zisizo za kawaida za uke.
10. UFANYAJI WA TENDO LA NDOA
May be true may be not, inategemeana na nguvu zenu ila wanawake wengine akifanya sana ndio anakuwa imara zaidi, wengine akifanya zaidi anakuwa legelege na uchi wake unakuwa mchafu - si unajua harufu ya shahawa
Pia kutumia nguvu kufanya tendo la ndoa wakati uke hauko tayari kufanya tendo hilo kunasababisha michubuko na hatimaye kuhatarisha uke kupata maambukizi hatari kwa haraka.
TAMBUA KIASI GANI KINAKUFAA KWA WIKI KWA AFYA YAKO usiige kwa wengine.