Tunoishi karibu na gesti house

Marketer

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
261
55
Kwanza naanza kwa kuwapa wanajamvi salamu zangu
leo nawapasha mambo yanatupata mitaa ya kawngu
Mwenzenu nilipopanga kuna gesti bubu jiarani yangu
Napambana na majaribu makubwa acheni tu ndugu zangu
Nitaftieni chumba mwenzenu wadau wangu singoji zamu yangu

Juzi nikakuta zogo watu wnamjia juu mwenye gesti yake
Nikaulizia, yapi yanamkuta mwenzangu na biashara yake
Iweje watu wajawe na hasira hadi waitake roho yake
Kumbe ule uchafu wa wateja zake autupa tu nje kwake
Hadipose vizuri ule uchafu wa zana za wateja zake

Mungu tuipushie waja si ndo juzi asubuhi kabwaga uchafu
Hamad watoto si wakaupitia na kchokoachokoa huo uchafu
Mama mmoja si akamuona mwanae anakuja akipuliza uchafu
kumfurumsha kwanini anapuliza zana za watu wa shetani mchafu
Mwenzie kadakia alikuta pulizo lina uji akaunywa wote kaninyima

Mama kajaza watu na kutinga pale gesti kulianzisha
Sasa mi nikajiuliza yule mtoto itakuwaje na hilo balaaa?
Toka juzi najiwazia, suluhisho ni kuhamia karibu na kanisa
Hivyo mnitaftie chumba wadau jirani na kanisa sasa
Bei ntatoa tu maana nimejione cheap is expensive sana
 
:happy: sio tu hivyo bali vyumba vya gesti havina sound proof aisee...yani miaka ya zamani kuna siku niliingiaga gest nikasema sitakaa niingie tena mule ndani...maana kila chumba unasikia makelele/sauti..mara kuna wanaogombana mara kuna wanaoibiana hela utasikia 'we usiponipa hela yangu leo tunauana' mara vyumba vingine ni makelele ya mahaba jamani, mi ningeshauri gesti zote zifungwe ni uchafu tu na ndio zinachangia kuongezeka kwa magonjwa...
 
Kukaa karibu na gesti haswa ukiwa na watoto ni kumkaribisha Shetani awe mwalimu wa familia yako.
 
:happy: sio tu hivyo bali vyumba vya gesti havina sound proof aisee...yani miaka ya zamani kuna siku niliingiaga gest nikasema sitakaa niingie tena mule ndani...maana kila chumba unasikia makelele/sauti..mara kuna wanaogombana mara kuna wanaoibiana hela utasikia 'we usiponipa hela yangu leo tunauana' mara vyumba vingine ni makelele ya mahaba jamani, mi ningeshauri gesti zote zifungwe ni uchafu tu na ndio zinachangia kuongezeka kwa magonjwa...

Utakuwa ulijichanganya ukaenda Guest za kulipia kwa sekunde
 
eh unanikumbusha huko tegeta karibu na jamaa yangu fulani kumefunguliwa guest house haina hata kibao lakini inajaa vibaya sana, ila tatizo ni hao wateja wanaenda kupaki gari zao nje ya nyumba ya hyo jamaa yangu halafu wanaenda guest kwa miguu, basi majani yake yote yamenyauka kwa pilika za kukanyagwa na magari muda wote nje kwake utadhani kuna sherehe au msiba kisa magari! anakazi ya kuzozana nao waondoe magari.
 
Back
Top Bottom