Tundu Lissu na Godbless Lema wapinzani pekee waliosimama kidete!

mcrounmj

JF-Expert Member
Feb 26, 2016
380
885
Hi great thinkers wote. Awali ya yote niwashukuru memba wa jukwaa hili kwa kuendelea kuleta maada moto kuelekea uchaguzi mkuu octoba 2020.

Tumeshuhudia kipindi kigumu mno cha siasa za upinzani. Kama ambavyo watawala wa nchi hii walikuwa wamedhamilia kuupoteza upinzani. Wapo waliofungwa, waliouawa, kupotezwa, kutekwa, na kupigwa risasi za moto.

Yote hayo ilikuwa ni kutekeleza ahadi ya kuua upinzani. Tumeshuhudia waliokuwa na mioyo myepesi wali surrender mapema na kujoin chama tawala, wapo pia waliosaliti kwa vipande vya shilingi!

Ila, miamba hawa wawili Tundu Lisu na Godbless Lema niliwahi kuwaongelea mwaka 2016, hata kabla ya tsunami iliyowakumba, ila mwisho wa siku wamedhihirisha ushujaa wao kwa kuhimili mawimbi makubwa ambayo yalikuwa yanatishia hata uhai wao.
 
Yamkini ww ni ant-ccm sasa tambua tu kwamba wapo videte maelfu kama Lisu na Lema, kwa hivo usibague
 
Kweli wapo makamanda wengi sana kama akina Mdee na yule wa Mara na wengine wengi akina Msigwa nk ni watu wakakamavu kabisa na wakusifiwa, kweli wamepigana.
 
Back
Top Bottom