"Tundu Lissu wa TFF" Wambura asahaulika gerezani .

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,231
Naona kimya kimetanda baada ya Michael Wambura kupewa kesi isiyo na dhamana kwa lengo la kumnyamazisha ili asifukue ushahidi kuhusu mla rushwa mwenye tuhuma nzito ndugu Wallace Karia.

Wadau taratibu wameanza kumsahau shujaa Wambura ambaye anatumikia "kifungo" cha kutengeneza gerezani.

Natoa wito kwa wanasimba wenzangu na wadau wa michezo nchini kuhakikisha Wambura anapewa msaada wa kisheria na kurejea uraiani .
 
Sir Leodgar Tenga alikosea sana pale alipopata nafasi ya urais na mwisho wa siku akashindwa kabisa kutengeneza katiba ambayo ingewabana wale wote wasio wanamichezo kugombea tff! Tff ilitakiwa iendeshwe na wachezaji wenyewe wa mpira waliostaafu na wenye rekodi na uadilifu uliotukuka.

Matokeo yake ndiyo haya! Ukimuangalia Jamal Malinzi na huyu mwenzake Wallace Karia, wote unaona lao moja tu! tofauti yao ni namna ya kula tu, mmoja alikula hadharani halafu huyu mwingine anakula kwa kujificha na pia kuwaharibia wengine kwa kigezo kuwa eti na yeye ni tii ai esi!
 
Naona kimya kimetanda baada ya Michael Wambura kupewa kesi isiyo na dhamana kwa lengo la kumnyamazisha ili asifukue ushahidi kuhusu mla rushwa mwenye tuhuma nzito ndugu Wallace Karia.

Wadau taratibu wameanza kumsahau shujaa Wambura ambaye anatumikia "kifungo" cha kutengeneza gerezani.

Natoa wito kwa wanasimba wenzangu na wadau wa michezo nchini kuhakikisha Wambura anapewa msaada wa kisheria na kurejea uraiani .
Ukienda kumsalimia gerezani mwambie aache dharau na mdomo, aache kujiona mwerevu kuliko watu wote anaisi atapiga dili watu wasielewe.
Mkumbushe hii ni awamu nyingine sio zile zilizopita.

Mfikishie hayo ukienda Segerea kumsalimia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom