figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Rais wa wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) Tundu Lissu, amesema utawala wake utahakikisha unainyoosha serikali ya awamu ya 5 ili ifuate misingi ya sheria.
Amesema hivi sasa nchi inakabiliwa na hali mbaya ya uvunjifu wa haki kutokana na baadhi ya viongozi kujiona wapo juu ya Sheria.
Akizungumza na Tanzaia Daima jijini Dar es Salaam, Lissu alisema katika utawala wake wa Mwaka mmoja, atahakikisha anashughulikia ipaswavyo kusimamia sheria.
Alisemahali mbaya ya Utawala wa Kisheria inasbabishwa na viongozi waliopo madarakani ambao wanawaonea wanyonge huku idara Muhimu za Kisheria ikiwemo Mahakama, Mawakili na Wapelelezi wakishindwa kufanya kazi kikamilifu.
"Kuna watu wanaamini wapo juu ya Sheria, niseme tu kuwa hakuna aliyea juu ya sheria sio rais wala Polisi, wanatakiwa wote wafuate sheria na hili ni kwa mjibu wa sheria na hata mimi mwenyewe kulisimamia hilo" alisema.
"Hivyo katika kipindi hiki nikiwa madarakani, nitajitahisdi kupiga kelele mambo yanayokiuka Misingi ya Sheria na Kamwe siwezi kuwa kimya" alisema.
"Mathalani nchi yetu imekuwa ikikumbwa na matukio kadhaa iliwemo hili la bashite ambalo TLS lazima ikemee kama ishara ya kusimamia misingi ya sheria" alisema.
Habari hii imeandikwa na gazeti la Tanzania Daima.
Swali ninalojiuliza ni ataanzia wapi kuinyosha? Manake kama ni kupinda haina mfano. Kuhusu Bashite ndo ashau kabisaa..!!