Tundu Lissu: Uchaguzi mdogo siku zote huwa ni mgumu upinzani kushinda

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
"Waheshimiwa na makamanda poleni kwa mapambano na hongereni kwa kazi kubwa mliyoifanya kwenye chaguzi hizi. Naona kila mmoja wetu anasikitika jinsi matokeo ambavyo yamekuwa tofauti na matarajio yetu na kazi tuliyoifanya. Ni rahisi, katika mazingira haya ya kushindwa na kabla vumbi halijaisha, kuanza kulalamika, kunyoosheana vidole na kukatishana tamaa. Hii haitusaidii sana. Badala yake, tunachohitaji zaidi ni 'brainstorming' kuliko 'blamestorming.'

Naomba nifanye ya kwanza. Chaguzi ndogo za ubunge au udiwani ni ngumu sana kushinda katika mazingira halisi ya nchi yetu. Mifano michache inathibitisha ukweli huu. Katika election cycle ya '05-'10, tulishinda Jimbo la Tarime lakini tukapigwa Biharamulo Magharibi na Busanda. Tarime lilikuwa Jimbo letu tangu Uchaguzi Mkuu wa '05, Busanda lilikuwa la maCCM na Biharamulo Magharibi lilikuwa la TLP.

Sikumbuki vizuri kama tulishinda Kata hata moja katika mzunguko wa uchaguzi wa kipindi hicho. Katika election cycle ya '10-'15, tulipigwa Igunga licha ya kazi kubwa tuliyofanya, lakini tukashinda Arumeru Mashariki iliyokuwa chini ya maCCM. Vile vile tulishindwa Kalenga, Chalinze na Ulanga Magharibi yaliyokuwa ya maCCM tangu Uchaguzi Mkuu wa '10. Kwenye chaguzi za Kata za '12 kama mnakumbuka, licha ya kazi kubwa na rasilimali nyingi, tulipata Kata tatu tu kati ya 26 zilizokuwa zinagombaniwa. Ukiachia Ifakara Mjini ya Mh. Juakali, Kata nyingine mbili - Kiboriloni na Iseke - zilikuwa zetu tangu Uchaguzi Mkuu wa '10.

Kwa mantiki hii, matokeo ya jana sio ya kushangaza sana. Kata ya Duru ilikuwa ya kwetu na tumeitetea, nyingine zote tulikopigwa zilikuwa za maCCM. Hatujanyang'anywa iliyokuwa yetu, hatujanyakua zilizokuwa zao. Hata hivyo, funzo kubwa zaidi la historia ya chaguzi hizi ni hili hapa: licha ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo hizi, tumeendelea kufanya vizuri zaidi katika kila Uchaguzi Mkuu uliofuatia kipigo cha chaguzi ndogo. Mwaka '10 tulifanya vizuri zaidi licha ya kupigwa Busanda na Biharamulo Magharibi katika mzunguko wa '05-'10. In fact, tulichukua Jimbo la Biharamulo Magharibi mwaka huo. Na tulipata Kata nyingi zaidi '10 kuliko ilivyokuwa '05. Mwaka '15 tulipata ushindi mkubwa zaidi katika Kata na majimbo licha ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo za mzunguko wa '10-'15. Hoja yangu hapa ni kwamba uchaguzi wa marudio hauna direct and negative bearing kwenye matokeo yetu ya Uchaguzi Mkuu unaofuatia. On the contrary, uchaguzi wa marudio unatupa fursa ya kupanda mbegu ambayo, ikitunzwa vizuri, inakuwa na mazao bora kwenye chaguzi zinazofuatia.

Kwa upande mwingine, chaguzi za marudio - kwa sababu ya udogo au uchache wa maeneo yanayogombaniwa - yanawapa maCCM fursa ya kutumia nguvu kubwa za rasilimali na za kidola ukilinganisha na tunazotumia sisi. Kwenye Uchaguzi Mkuu unaofuatia, nguvu hizo zinasambazwa nchi nzima na kwa hiyo effectiveness yake inapungua. Ndio maana tumefanya vizuri zaidi kwenye Uchaguzi Mkuu kuliko kwenye chaguzi ndogo za marudio. Hili, kwa maoni yangu, ndilo fundisho kuu la chaguzi hizi za marudio. Hatuna sababu kubwa ya kushangilia kutokana na matokeo ya jana. Hata hivyo, hatuna sababu yoyote ya kuomboleza pia. Obviously, maCCM na wapambe wao wataandika 'wasifu wa marehemu' wa CHADEMA/UKAWA na kuutangaza dunia nzima na kwa sauti kubwa. Hilo lisitupofushe macho yetu, hata kama linakera sana.

Tutathmini kazi tuliyoifanya na matokeo tuliyoyapata. Tupate mafundisho sahihi ya kazi hiyo na matokeo yake. Tutumie mafundisho hayo kwa kujipanga vizuri zaidi kwa ajili ya 'the real prize': 2020. Nawatakieni alfajiri njema."
 
Nilikua najaribu kupitia baadhi ya matokea ya maeneo mbali mbali, ila nilichonote ni kwamba CUF na CHADEMA kwenye hayo maeneo ni Wengi, ila kukosa ushirikiano,

Ama hakika umoja ni nguvu,
Kiukwel sijaelewa mantiki halisi ya kuwa na UKAWA alaf sehemu wanasimama wagombea wawili wa vyama vinavyounda UKAWA ( yaani enei moja anasimama mgombea wa CDM na mgombea wa CUF) ,

Mfano: ccm -6, cdm-4 , cuf-3
Hivi kwa scenario kama hii
Ingekua cdm + cuf= ukawa
then 4+3=7 , je c ushindi huo?

Kiukwel wapinzani bila kupepesa mdomo tuna safari ndefu sana ya kuitoa ccm madarakani.

Ni mtazamo wangu tu
 
Huu ni uongo wa hali ya juu kutoka kwa huyu jamaa self proclaimed mwanasheria nguli, inabidi aseme ukweli wanapoteza muda mwingi kumtukana rais bila kuwaeleza watanzania ni watakifanya. CCM haina sababu ya kuiba kura wakati inasaidiwa na wapinzani wenyewe kuipatia nguvu. Mwezi mzima wameng'ang'ania njaa njaa njaa, walianza na UKUTA UKUTA UKUTA hivi wananchi japo wanadanganywa na CCM lakini wanaona hakuna mbadala wa ccm. Katika kampeni zao badala ya kuishitaki CCM kwa wananchi wanang'ang'ania kumtukana rais ambaye kwa aina Fulani kishajikita mioyoni mwa watanzania japo ki utapeli kama Lowasa walivyojikita mioyoni mwa wana mitandao ambao wengi wao hawapigi hata kura. CHADEMA ni chama kinachotuangusha watanzania na mategemeo yote tuliyokuwa nayo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana yanaanza kwenda na maji sababu ya kuwa na uongozi wa kinafiki na kihuni. Mijitu iliyotufikisha hapa tulipo katika ngazi mbalimbali za serikali ndiyo tunawapa dhamana ya kutupeleka katika mabadiliko ni wajinga peke yao watawaelewa kina Lissu. Sumaye anawaambia nini watanzania kuwa ccm ni wezi, wamedumaza maendeleo yetu? Akiulizwa yeye alifanya nini wakati akiwa mmoja wao atajibu nini. haiiniingii akilini mwangu watu wanaojiita wa GT hapa JF wakirubuniwa kitoto namna hivi.

Mabadiliko makubwa katika CHADEMA na vyama vingine vya upinzani yanatakiwa kabla ya kufikiri kuingia Ikulu,
 
Mbona 2008 Tarime mlishinda?

Kamanda jipangeni tu acheni blah blah
 
Vizuri ila ikikumbe kuzifanyia kazi tafiti zitolewazo sio kuzipuuza.Walofanya wanakustua na unatakiwa tujiulize tufanyeje kelele nyingi bila mipango mtasingizia kila siku mnaibiwa na uchaguzi haukuwa huru pale mshindwapo mnaposhinda ulikuwa sawa....MI NINACHOONA HAMKO SERIOUS NA KUCHUKUA DOLA, mnafanya siasa uchwara tu
 
Msiwe na wasiwasi hata 2020 mtatetea Viti vyenu, CCM nao watatea viti vyao ikiwemo kitu cha urais.
CCM wamtawala inchi kwa miaka hamsini, wanaposhinda Kara ishirini hlf ww unashinda kimoja, then unatamba eti Haman shida kwakuwa wametetea vitu vyao 20 ww umetetea kitu chako kimoja bac huo ni umbulula!!
 
uchaguzi wa marudio wa Arumeru Mashariki ccm ilitumia nguvu kubwa ikiwemo ya kurubuni baadhi ya wazee wa kimila wakiongozwa na Edward Lowasa ambaye alikuwa anampigia debe mkwe wake lakini wote tunakumbuka Chadema wakati huo chini ya Dr. Slaa ilivyowasambaratisha huku ukiacha gumzo la rais mstaafu Mkapa na Vicent Nyerere wakitupiana vijembe mmoja akisema vicent hatambuliki kwenye ukoo wa Nyerere mwingine akimshutumu Mkapa kuhusika na kifo cha Nyerere hivyo hoja za Tundu Lissu hazina mashiko
 
Huu ni uongo wa hali ya juu kutoka kwa huyu jamaa self proclaimed mwanasheria nguli, inabidi aseme ukweli wanapoteza muda mwingi kumtukana rais bila kuwaeleza watanzania ni watakifanya. CCM haina sababu ya kuiba kura wakati inasaidiwa na wapinzani wenyewe kuipatia nguvu. Mwezi mzima wameng'ang'ania njaa njaa njaa, walianza na UKUTA UKUTA UKUTA hivi wananchi japo wanadanganywa na CCM lakini wanaona hakuna mbadala wa ccm. Katika kampeni zao badala ya kuishitaki CCM kwa wananchi wanang'ang'ania kumtukana rais ambaye kwa aina Fulani kishajikita mioyoni mwa watanzania japo ki utapeli kama Lowasa walivyojikita mioyoni mwa wana mitandao ambao wengi wao hawapigi hata kura. CHADEMA ni chama kinachotuangusha watanzania na mategemeo yote tuliyokuwa nayo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana yanaanza kwenda na maji sababu ya kuwa na uongozi wa kinafiki na kihuni. Mijitu iliyotufikisha hapa tulipo katika ngazi mbalimbali za serikali ndiyo tunawapa dhamana ya kutupeleka katika mabadiliko ni wajinga peke yao watawaelewa kina Lissu. Sumaye anawaambia nini watanzania kuwa ccm ni wezi, wamedumaza maendeleo yetu? Akiulizwa yeye alifanya nini wakati akiwa mmoja wao atajibu nini. haiiniingii akilini mwangu watu wanaojiita wa GT hapa JF wakirubuniwa kitoto namna hivi.

Mabadiliko makubwa katika CHADEMA na vyama vingine vya upinzani yanatakiwa kabla ya kufikiri kuingia Ikulu,
kuna vitu vingi nakubaliana na wewe! ukweli CHADEMA kwa sasa wanakera wamekuwa watu wazima moto na matokeo yake hayaleti mafanikio.
kikubwa tunachoweza kuwashauri ni kwamba haijalishi wamekosea wapi na mara ngapi, bali warudi wajipange upya ili tuweze kuwapa dhamana tuliokuwa tumewapa mwanzo.
kiukweli toka lowasa ameingia amewachanganya walitegemea wangemtumia kwa wao kuongeza viti vya bunge na kujijenga kisiasa zaidi na kwa kweli hilo lilifanikiwa na kupata kura nyingi sana. lakini inaonyesha wazi kabisa hawamwitaji tena katika chama chao na wangesikia faraja kama angesema kwa hiyari yake kuwa anajiuzuru siasa au hatagombea ila atakuwa mfadhiri na mshauri wa chama hii ndio nafasi wanayotaka.
tabu ni pale inapokuja hioyo yao haimtaki na hasa viongozi kwa kuwa wanaujua ukweli kuwa kwa kwa 2020 hatauzika, lakini nani wanamuweka hilo ni lingine mtu anayeweza kukibeba chama anaoneka ni huyu tundulisu lakini na yeye sio wa kwetu anaweza kutugeuka asiimbe au kuruka kama tunavyotaka.
matokeo yake bado hawajakaa kusema ukweli uelekeo ya 2020 ni upi na nani anaweza kusimama.
 
Wasipokua na muungano imara na wenye uimara watalia miaka yote kwa nchi zetu za kiafrica kukishinda chama tawala kunaitaj umoja usio na undumilakuwil
 
Hapo mimi nitatofautiana na nguli Tundu Lissu:
Ishu hapa ktk uchaguzi huu wa jana uliopita pamoja na mapungufu mengine mengu lukuki lakini tatizo kubwa ipo kwa wapinzani wenyewe.
Wapinzani chini ya mwamvuli wao wa"UKAWA" wslipaswa kusimamisha mgombea moja moja katika kila kata nchi nzima, lakini hawakufanya hivyo.
Takwimu za uchaguzi huu unaonesha kwamba Wapinzani wenyewe wamesimamisha wagombea wa vyama vyao katika kila kata wakagawana kura na kuwarahisisha CCM kushinda kirahisi.
Je,,ni kwanini Wapinzani hawakuweza kukaa pamoja na kusimamisha mgombea moja moja kila kata? kwanini wameendelea kubaki na uvyama wakati wana Mwavuli wao wa "UKAWA"
Je ni lini sasa wapinzani warakuwa wamoja na kuacha itikadi na ubinasi wa vyama vyao?
Kama kweli wapinzani wanahitaji ushindi dhidi ya CCM ni bora wakakubali kuungana kwa umoja wao,, waachane na ubinafsi, chuki na unafiki wa kivyama kama kweli wanataka kuishinda CCM. waache kutanguliza uvyama wao kwanza bali waunganishe nguvu kabisa...na kuweka kando ubinafsi na chuki zao za kivyama.
Kuishinda CCM si lelemama, inahitaji kujifunga mkanda kwa umoja na kupanga vyema na kusonga mbele ktk umoja imara na dhabiti....
Itikadi na ubinafsi ya uvyama ktk vyama vya upinzani na uchu wa madaraka katu haitoitoa CCM madarakani.
Mimi binafsi siitetei CCM na kamwe sitokaa niitee CCM lakini nawapa changamoto wapinzani kuwa kabla hatujaanza kuilalamikia CCM kuwa wao wanabebwa na Tume mbovu ya uchaguzi na vyombo uya dola ni bora tukajiuliza pia kwa upande wetu, je sisi tumejipanga kiasi gani katika umoja wetu wa UKAWA?
Kwanini katika umoja huo tunashindwa, na tumeendelea kushindwa kusimamisha mgombea moja moja katika kila kata?
Ni wakati wa kuacha kuilalamikia CCM kuwa wanabebwa na vyombo vya dola na tume mbovu ya uchaguzi wakati sisi wenyewe wapinzani hatujajipanga vilivyo katika umoja wetu....Umoja wetu uwe dhahiri kwanza,,,halafu ndio tuilalamikie rafu na ubebwaji wa CCM katika chaguzi.
Wapinzani tusipowaza hayo,, na kuifanyia kazi vilivyo,,kuishinda CCM ni sawa na ndoto za Alinacha, ,,kamwe haiji, ,,na haitakuwa,,,,
Tujifunze pia katika uchaguzi wa mwaka jana uliopita wa Rais,, Wabunge na madiwani.... Katika baadhi ya majimbo(Sio chache) wapinzani walipoteza majimbo hayo kwa kuwasimamisha wagombea kwa kila chama kupitia katika vyama vyao, hasa CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI wakishindana na CCM.
hapo walichofanya wapinzani ni kugawana kura na kuiachia CCM njia nyeupe kuishinda kirahisi, mfano wake ni Jimbo la UKONGA na jimbo L MWANGA na majimbo mengine kwa kutaja tu kwa uchache.
Tulipaswa kujifunza juu ya hilo, lakini katika uchaguzi huu wa marudio tumeendelea kufanya makosa yale yale huku tukifikiri kuishinda CCM ni kazi rahisi...
Kwanini tunashindwa kujifunza kutokana na makosa? na je, kama hatufanyi marekebisho katika makosa hayo, ni nini maana ya kuwa katika Mwamvuli wa UKAWA?
Wapinzani tujipange....tusiendelee kulalamika wakati wachawi ni sisi wenyewe ndani ya vyama vyetu. Tuachane na ubinafsi, chuki, uchu wa madaraka na unafiki katka vyama vyetu.Tusipoachana na hayo yote kamwe hatutoweza kuisjinda ccm katika chaguzi,,,,,CCM wataendelea kushinda kila chaguzi.
Tubadilike tufanye kazi kimkakati tuunganishe nguvu kwa pamoja, takwimu za miaka iliyopita haitotusaidia sana,,,
Tunahitaji kubadilika kifkra/kimtazamo na tujione wamoja katika vyama vyetu badala ya kujiona UCHADEMA, UCUF nk,.
Tunahitajika tujione katika umoja wetu Kama UKAWA tunaposhindana na CCM katika chaguzi, bila hivyo tutaendelea kuimba wimbo wa kuonewa, kuibiwa na kuchezewa rafu katika chaguzi. Jambo la msingi kabisa tunapaswa kujiuliza, je sisi kwanza tumefanya nini kabla ya kuanza kulalamika? je ni kweli tumeachana na chuki na ubinafsi ndani ya vyama vyetu? je tumekubali kweli kuwa wamoja na kuheshimiana kwanza kwa itikadi zetu? Je,,kweli tupo tayari kushirikiana Sawia kabla ya kutoka nje ya Umoja wetu wa UKAWA ili kushindana na CCM?
NAOMBA TUJISAHIHISHE, KUISHINDA CCM SI LELEMAMA, TUKAJIPANGE UPYA BADO HATUJACHELEWA SANA. HATA SASA INAWEZEKANA KAMA KWELI KUNA NIA YA DHATI.
 
Tundu NA maCDM wenzake kila wakishindwa wanatuletea hadithi ya sungura NA zabibu.

Words are very cheap. Action speaks
 
Kamanda, naona leo upo hapa kutetea kushindwa kwenu, umeanza na bandiko la Mtatiro na sasa la Lisu yawezekana yapo mengine sijayaon mimi. Poleni sana.

Halafu ukitoka hapa unakwenda kuwaambia watu 2020 CCM hawatoki, wakati kipimo cha uchaguzi mkuu ni hizi chaguzi ndogo ambazo mnaangukia pua kila uchwao. Kubalini kubadili mbinu badala ya kukaa mkidanganyana watu wazima na kujipa matumaini hewa.
 
hahahahaha ooooh tumetea kiti ooooh CCM nao wametetea viti vyao hahaha
Kwa hiyo hata uchaguzi wa mwaka 2020 CCM watatea kiti chao na hasa kiti cha Urais...
Kwa hiyo mlienda kutetea kiti chenu tuu na huo ndio ulikuwa mkakati wenu hahahaha
 
Nilikua najaribu kupitia baadhi ya matokea ya maeneo mbali mbali, ila nilichonote ni kwamba CUF na CHADEMA kwenye hayo maeneo ni Wengi, ila kukosa ushirikiano,

Ama hakika umoja ni nguvu,
Kiukwel sijaelewa mantiki halisi ya kuwa na UKAWA alaf sehemu wanasimama wagombea wawili wa vyama vinavyounda UKAWA ( yaani enei moja anasimama mgombea wa CDM na mgombea wa CUF) ,

Mfano: ccm -6, cdm-4 , cuf-3
Hivi kwa scenario kama hii
Ingekua cdm + cuf= ukawa
then 4+3=7 , je c ushindi huo?

Kiukwel wapinzani bila kupepesa mdomo tuna safari ndefu sana ya kuitoa ccm madarakani.

Ni mtazamo wangu tu
Upo sahihi mkuu! Ila katika kuliweka hilo sawa lazima profeseli aondolewe hata kwa kutumia njia ya mapepo,bila hivyo huyu jamaa atagawa kura 2020
 
Upo sahihi mkuu! Ila katika kuliweka hilo sawa lazima profeseli aondolewe hata kwa kutumia njia ya mapepo,bila hivyo huyu jamaa atagawa kura 2020
Ni kweli aisee yan huu mgongano na utengano unaosababishwa na Pro-pesa ni bonge la weakness na Ccm wanalitumia vizur.

The only way ni kuungana kwa dhati,
 
Ni kweli aisee yan huu mgongano na utengano unaosababishwa na Pro-pesa ni bonge la weakness na Ccm wanalitumia vizur.

The only way ni kuungana kwa dhati,
Wewe unafikiri hata yule mwandikishaji wa vyama vyetu ujasiri wa kupeleka pesa kule anautoa wapi? Ametumwa na lile kundi la maharamia kutupola umoja wetu,Huo ni mkakati mkubwa sana dawa ni moja tu kumpinga la profeseli mpaka ndani ya shimo la mapumziko.
 
Back
Top Bottom