kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,428
- 13,936
Watanzania tuko 50 milioni lakini tuko kwenye makundi mbali mbali yanayotuunganisha zaidi ya kifamilia, kiukoo, kikanda, kidini, kijinsia, kitaaluma, kiofisi na kikazi.
Makundi haya yanajisikia kuwa karibu zaidi kuliko watanzania wengine wote nchini.
Hivyo maumivu, manyanyaso, maonevu na mateso ya mwanakikundi mwenzao ni yao pia na adui ya mwanakikundi mwenzao ni adui yao pia; hivyo watafanya kila kiwezekenacho ili kumfariji mtu wao.
Tundu Lissu kushinda urais wa TLS ilitokana na dhana hii, wanasheria bila kujali tofauti zao waliungana nyuma ya taaluma yao kumfariji mwenzao.
Hali ndo hiyo hata kwa makundi mengine kama vile wabunge, polisi, wanajeshi, wanawake, manesi, walimu, n.k. Maumivu, manyanyaso au maonevu ya mwenzao ni maumivu yao pia.
Jamii na wanakundi husika wana uwezo kamili wa kufahamu kama mwenzao anatendewa haki au anaonewa tu anavyofanyiwa. Kama wakihisi kuwa alionewa wataungana naye kwa hali na mali kinyemela au kwa uwazi. Hiki ndicho kilichotokea kwa TL na TLS, hatuna budi kujifunza somo hili ili kuepukana na uchungu wa mwana aujuae mwanakikundi.
Mfano, wabunge wote duniani wajihisi na kujiona watu wenye thamani na heshima kubwa ndani ya jamii, hivyo kukamatwa na kulala mahabusu bila utaratibu wanajihisi kushushiwa hadhi yao bila kujali vyama vyao, na hasira zao bila kujali vyama utaiona siku ikifika.
Hivyohivyo hata kwa makundi mengine ya mfanano.