MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Godbless Lema anatuma ujumbe unaosema, msihangaike kutaka nipate dhamana kwa sababu watawala wameamua nikae mahabusu mpaka watakapopenda nitoke.
Tundu Lissu anajitokeza anatuambia Lema yuko mahabusu kwa sababu ya maelekezo kutoka kwa mamlaka ya juu iliyoishinikiza mahakama kumuweka mahabusu bila kupewa dhamana wakati sheria inaitaka mahakama kumpa dhamana.
Mwanasiasa huyo huyo, Tundu Lissu anajitokeza tena baada ya wiki kadhaa kupita na kuanza kusema, tunaongeza jopo la mawakili wa Lema ili tuhakikishe anapata dhamana na kushinda kesi zake.
Kwa mtu mwenye kuchambua mambo unajiuliza, kuna umuhimu gani wa kuongeza mawakili wakati ulituambia uwepo wa Lema mahabusu sio kwa sababu ya takwa la sheria bali kwa sababu ya agizo kutoka kwa watawala. Kuongeza mawakili kutasaidia nini wakati sheria hazina nafasi katika kesi ya Lema!
Unahitimisha kwa kusema, Kama kungekuwa na shinikizo kutoka kwa watawala linaloweka sheria kando basi kwa watu wanaojitambua wasingehangaika kuongeza jopo la Mawakili bali wangehangaika kuongeza joto la kisiasa ili sheria zilizowekwa kando na mahakama zifanye kazi.
Waingereza wana methali isemayo, ‘’You can't have your cake and eat it too’’.
CHADEMA wanatakiwa wachague moja kati ya madai yao kwa sababu wakichagua mambo mawili kwa pamoja hayaleti mantiki kifikra na katika uhalisia.
CHADEMA watuambie either Lema hajapata dhamana kwa sababu ya mapungufu kutoka kwenye jopo la Mawakili wake AU hajapata dhamana kwa sababu mahakama imepata maelekezo kutoka watawala lakini siyo kwa sababu ya vyote kwa pamoja.
Ni sawa na mwanasiasa anakuambia wasimamizi wa uchaguzi wanatangaza mshindi bila kuhesabu kura zetu kwa sababu wameamliwa na mamlaka ya juu. Halafu baadaye anakuambia tena tujitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na tutashinda.
CHADEMA waache kujificha kwenye hoja zenye logical fallacies.
Unaweza kwenda mbele zaidi na kusema, wanasiasa wanajaribu kuingiza siasa kwenye masuala ya kisheria wakati sheria hazina siasa. Lema ataendelea kusota mahabusu huku wakipiga siasa ambazo hazitaleta mafanikio katika kesi yake.