Tundu Lissu 'haifahamu vyema' Tanzania

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,858
Mbunge wa Singida Mashariki,Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA,Wakili Msomi Tundu Antipas Mughway Lissu haifahamu vyema Tanzania na watanzania wake. Kila anaposimama Bungeni kuhutubia au kuwasilisha hoja,huzua mjadala nchi nzima. Watanzania wengi huishia kusema Lissu ametukana,amedharau au amepotosha.

Watanzania,tangu kupata uhuru,wana mambo yao wanayataka kuyasikia au kuyaona. Wanataka kusikia watawala wakisifiwa na si kukosolewa kwa ajili ya kuboresha nchi yetu. Watanzania wanataka kusikia na kuona mambo mepesimepesi na si mazito ya Lissu.

Hoja za Lissu hujaa taarifa za kitafiti na kuunganisha matukio kisomi halafu hutoa ushauri au angalizo. Taarifa za Msomi Lissu hutaja wahusika wa kupotoka kwetu kama watanzania bila kuficha hata herufi moja. Watanzania hawataki mambo magumu ya Lissu,yaani mambo yaliyojaa ukweli ambao ulifichwa au kupotoshwa.

Kutokana na ugumu wa hoja za Lissu,Lissu huanzia Bungeni hadi mtaani kukosolewa,kushambuliwa na kukejeliwa badala ya kufanyika tafakuri ya kutosha kwa hoja zake firikishi. Lakini,Lissu huwa haachi. Anapopata tena nafasi,huendelea na somo lake gumu na chungu la kuanika ukweli usiopendwa.

Ndiyo maana nasema Lissu haifahamu Tanzania na watanzania wake. Hawataki vya kufikirisha ila wanataka ya kufurahisha. Mambo ya kisheria ayapendayo Msomi Lissu ni magumu na 'yanakera' ingawa ni muhimu katika kujisahihisha.
 
Nikutie moyo hao wasiomuelewa Lisu ni baadhi ya maCCM wenye kushikiloiwa akili na Lumumba (rejea bandiko #4 kuthibitisha hoja yangu). Mbona watanzania tulio wengi tunaelewa anachosema; na watawala usipime wanaelewa ila wakufa na tai shingoni.
 
CCM ya 2016 imekuwa sawa na Chadema ya 2007 na Chadema ya 2016 Imekuwa sasa na CCM ya 2007!
Tundu Lissu anataka Ndugu Rais atafute vifungu vya sheria kumfukuza Meneja Bandari wakati huo Makontena ya wafadhili wao yanapita bure! Udhibiti wa Upotevu wa Mapato bandarini huenda ndio yameyeyusha harambee!
 
Tatizo tuna wasomi wenye vyeti na viongozi wasiojua kazi zao. Raia nao wamekuwa watu wa matukio.
Mtu anaweza kuwa anafanya jambo ambalo ni zuri lakini likawa kinyume na sheria na taratibu zilizopo.
Lissu, anaeleza yote haya kwa uwazi lakini hakuna anayetaka kuelewa, kwa kuwa wengi walishabinafsisha akili na hivyo yupo mtu anafikiria kwa ajili yao.
 
unaposema lissu anatoa "taarifa za kiutafiti" kwa hiyo tuamini kuwa kwl lowaxa ni fisadi? maana ni huyu huyu mwanasheria msomi tundu lissu ndiye alikuwa akituimbia kuwa lowasa ni bingwa wa mikataba ya kifisadi.
 
unaposema lissu anatoa "taarifa za kiutafiti" kwa hiyo tuamini kuwa kwl lowaxa ni fisadi? maana ni huyu huyu mwanasheria msomi tundu lissu ndiye alikuwa akituimbia kuwa lowasa ni bingwa wa mikataba ya kifisadi.
Hapo sasa ndio utawataka ubaya
 
Petro E. Mselewa, majibu mengi unayopewa humu yanazidi tu kuthibitisha hayo unayosema...ni kweli kuwa uelewa wa Watanzania walio wengi ni mdogo sana. Wachache wenye uelewa kiasi unafiki umewetawala mioyo yao na ulafi matumbo yao. Wamebaki wanatumia ushabiki wao kuliko akili na bahati mbaya hata jamvi letu hili halikupona.

Ukiwauliza hawa watu kwa nini Magufuli angalau haipi hoja ya Katiba mpya kipaumbele ili hatua zake zipate nguvu kisheria hawana majibu. Inakuwaje watu waliopinga Rasimu ya Katiba ya Warioba sasa wachangamkie kukurupuka kwa viongozi bila kuzingatia sheria zinasemaje? Huku ni kuonesha kiwango cha kutisha cha ulemavu wa fikra.

Kwa upande wangu nitazidi kumuomba Mh. Tundu Antipas Lissu asichoke na azidi kutoa elimu kwani gharama za ujinga siku zote ni kubwa sana. Utalaumuje dhambi za watumishi wa awamu zilizopita huku unajua vitendo vyao vilikuwa na baraka za Viongozi wao wakuu ambao kama Katiba ingeruhusu, wangetakiwa kutangulia Keko.

Mkapa anatamba mitaani akiwa huru na Kikwete anapeta mitaani akiwa huru, huku kila moja anajua wao ndio walikuwa vinara wa ufisadi nchini. Fikiria Rais wa nchi anajimilikisha migodi wa Kiwira, Rais anaingia madarakani kwa hela ya wizi na rushwa au Rais anaiingiza nchi kwenye mkataba mkubwa wa umeme nchini na kampuni hewa!

Lakini baya kupita yote, ni chama tawala kujimilikisha miradi, rasilmali za taifa na mali za wananchi bila ridhaa yao na kuzitumia kwa manufaa ya wachache. Kama Magufuli angekuwa na dhamira ya kweli kulinusuru taifa hili kutoka kwenye tope la maovu angeanza kwa kutuomba radhi, tumsamehe yeye na chama chake halafu tuanze upya.

Ukitaka mti ufe kabisa na usije ukachipuka tena unahakikisha umekata mizizi na siyo matawi kama anavyofanya Magufuli, hapana, huu ni usanii. Huanzi kujenga ukuta wa nyumba, unajenga msingi kwanza unaoweza kustahimili uzito utakaotua juu yake...Magufuli tafadhali, fufua mara moja mchakato wa Katiba mpya, Rasimu ya Warioba.
 
Back
Top Bottom