VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kimya kingi kina mshindo mkuu. Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amejipanga kulitikisa Bunge na Taifa kwa ujumla kuanzia tarehe 26/1/2016. Tarehe tajwa ni terehe ya kuanza kwa vikao vya Bunge la 11. Hiyo itafuatia kuundwa kwa Kamati za Kibunge zitakazotangazwa tarehe 20/1/2016 na Spika Job Ndugai.
Lissu, kwa muda mrefu sasa, amekuwa kimya. Taarifa za kiintelijensia na za kuaminika, zinaonesha kuwa Lissu alijichimbia kufanya tafiti na matayarisho kwa ajili ya kulitikisa Bunge kupitia Hoja yake Binafsi anayotarajiwa kuiwasilisha Bungeni Dodoma. Lissu anadhamiria kukumbushia sakata la Escrow na kuonesha jinsi Bunge 'lilivyopuuzwa'
Mbunge Lissu ni kati ya Wabunge wachache nchini ambao wakiongea huacha mjadala kwakuwa husema kile anachokiamini hata kama kitagusa au kukwaza wasikilizaji. Taarifa zinaonesha kuwa Lissu atasaidiana na Wabunge wengine wa CHADEMA na CUF 'kulipua' bomu linalohusu wizi wa makontena Bandarini pamoja na mkataba tata na wenye maumivu hasa wa IPTL.
Rais Magufuli ajiandae kuwa na wasaidizi wa kutumbua majipu. Stay tuned!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam