Tundu Lissu aomba msaada CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,025
164,289
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), amewataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushirikiana na wabunge wa upinzani kutunga sheria nzuri.

Aidha, Mbunge huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amekosoa kile alichokiita utungaji wa sheria kwa nia ya kuwakomoa wapinzani kwa kuwa anaamini ipo siku hata CCM zitawakandamiza watakapokuwa na makosa.

Lissu aliyasema hayo katikati ya wiki iliyopita wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bungeni mjini hapa.

Katika maelezo yake, Mnadhimu Mkuu huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alilalamikia sheria tatu zilizopitishwa na Bunge kwa nyakati tofauti, kwamba hazikustahili kupitishwa na chombo hicho.

Alizitaja sheria hizo kuwa ni Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektoniki.

Lissu alidai Bunge limekuwa likipitisha sheria zisizostahili kwa kutokana na wingi wa wabunge wa chama tawala. Alisema watalawa wanapaswa kukumbuka kuwa sheria hizo zinaweza kuwaumiza siku za usoni kama ilivyo kwa mmoja wa marais wa Ghana aliyepitisha sheria ya kuwaweka watu kizuizini na baadaye sheria hiyo ikatumika dhidi yake.

"Ninyi mlio wengi mkinyamaza, jana ni sisi, leo ni Nape (Nnauye) na kesho ni ninyi. Tafadhalini waheshimiwa wabunge, haya mambo mabaya yanayofanyika nchini, mtashughulikiwa ninyi wenyewe baada ya sisi kushughulikiwa na hakutakuwa na mtu wa kuwasemea maana na sisi tutakuwa tumefungwa," alisema.

"Kuna vitu vinaonyesha tumejisahau.

Katiba ya Kenya ya sasa, vile vifungu vya mwanzo kabisa vinazungumzia alama za taifa. Sisi leo tuna huu ni mwaka wa 66 tangu tupate uhuru. Kwa sheria za Tanzania Waziri atueleze kama Wimbo wa Taifa unatambuliwa kisheria."

Chanzo: Nipashe
 
Ungelinunua kwanza halafu ndio uanzishe hii thread. Una uhakika utakuta hayajaisha?!
 
Nilifikiri msaada kwa ajili yake mwenyewe, kumbe ni msaada wa kutunga sheria nzuri kwa manufaa ya watanzania wote bila kujali chama.
Ungeboresha heading ya uzi wako ingekua nzuri zaidi.
Mfano "Tundu lissu (mb chadema) amewataka wabunge wa CCM kushirikiana na wabunge wa upinzani kutunga sheria nzuri"
Ingekuwa ndefu sana
 
Wewe nawe fala kweli! sasa hapo maji ya shingo yako wapi? Tundu kasema ukweli! bora ungenyamaza ufiche ujinga wako! usiwe mvivu ws kufikiri!
Punguza povu kamanda.Tundu hawezi ndio maana anawaomba ccm,mbona alichoweza kukifanya hakuomba msaada wa ccm
 
Wala sio msaada ila huo ni wajib wa wote kusimamia maslahi ya wapiga kura wao na kutunga sheria ambazo sio gandamizi
 
Wewe nawe ! sasa hapo maji ya shingo yako wapi? Tundu kasema ukweli! bora ungenyamaza ufiche ujinga wako! usiwe mvivu ws kufikiri!
Tatizo kubwa ka JF kumejaa watu tunaowaita misukule ya vyama. Lissu kaongea jambo la maana sana hapa lakini wafuasi wanaanza kuchambana kwaajili limeongelewa na Lissu.

Kuna sharia nyingi sana za kijinga huhitaji hata kuwa mwanasheria kujua zilipitishwa na watu wehu kama baadhi ya wachangiaji huku JF. Nilichokipenda Lissu katumia busara ya kujaribu kuunganisha wabunge wa CCM na Upinzani kuwa kitu kwa kutumia lugha ya kiuungwana. Lakini sababu humu JF misukule ni mingi itamkashfu. Halafu tabia ya mafali waiwili hawakai zizi moja nadhani hatuielewi Lissu kaamua kuwe na fahari moja ili kufanikisha muungano wa wabunge....

TUZIMBEZE na WALA TUSIJIGAMBE bali tumuunge mkono kwa kuchangia hoja ya maana bila kumkatisha tama.
 
Nilifikiri msaada kwa ajili yake mwenyewe, kumbe ni msaada wa kutunga sheria nzuri kwa manufaa ya watanzania wote bila kujali chama.
Ungeboresha heading ya uzi wako ingekua nzuri zaidi.
Mfano "Tundu lissu (mb chadema) amewataka wabunge wa CCM kushirikiana na wabunge wa upinzani kutunga sheria nzuri"
Au angeandika heading kwamba CCM kukiona cha mtema kuni siku za usoni.....
 
Tatizo kubwa ka JF kumejaa watu tunaowaita misukule ya vyama. Lissu kaongea jambo la maana sana hapa lakini wafuasi wanaanza kuchambana kwaajili limeongelewa na Lissu.

Kuna sharia nyingi sana za kijinga huhitaji hata kuwa mwanasheria kujua zilipitishwa na watu wehu kama baadhi ya wachangiaji huku JF. Nilichokipenda Lissu katumia busara ya kujaribu kuunganisha wabunge wa CCM na Upinzani kuwa kitu kwa kutumia lugha ya kiuungwana. Lakini sababu humu JF misukule ni mingi itamkashfu. Halafu tabia ya mafali waiwili hawakai zizi moja nadhani hatuielewi Lissu kaamua kuwe na fahari moja ili kufanikisha muungano wa wabunge....

TUZIMBEZE na WALA TUSIJIGAMBE bali tumuunge mkono kwa kuchangia hoja ya maana bila kumkatisha tama.
Ifike muda tuwetuangalia utaifa wetu zaidi! nasio vyama vyetu! niaibu kupitisha sheria za hovyo, wakati tunawanasheria wazuri! wanaosifika kimataifa! tuweke mbali vyama vyetu kwenye mambo ya msingi!
 
johnthebaptist: Hivi kama hicho alichokisema Lissu ungepewa kwenye mtihani wa 'Ufahamu' kidato cha Nne au Sita na baada ya kusoma habari hiyo ukapewa swali la kupendekeza kichwa cha habari ungeandika hiki kichwa ulichoandika? Kweli CCM inapendwa na watu wenye Elimu mgogoro. Kichwa cha habari hakiendani na habari yenyewe. Sasa hapo msaada gani alioomba?
 
Tatizo kubwa ka JF kumejaa watu tunaowaita misukule ya vyama. Lissu kaongea jambo la maana sana hapa lakini wafuasi wanaanza kuchambana kwaajili limeongelewa na Lissu.

Kuna sharia nyingi sana za kijinga huhitaji hata kuwa mwanasheria kujua zilipitishwa na watu wehu kama baadhi ya wachangiaji huku JF. Nilichokipenda Lissu katumia busara ya kujaribu kuunganisha wabunge wa CCM na Upinzani kuwa kitu kwa kutumia lugha ya kiuungwana. Lakini sababu humu JF misukule ni mingi itamkashfu. Halafu tabia ya mafali waiwili hawakai zizi moja nadhani hatuielewi Lissu kaamua kuwe na fahari moja ili kufanikisha muungano wa wabunge....

TUZIMBEZE na WALA TUSIJIGAMBE bali tumuunge mkono kwa kuchangia hoja ya maana bila kumkatisha tama.

Tundu Lisu ni retarded!
 
Punguza povu kamanda.Tundu hawezi ndio maana anawaomba ccm,mbona alichoweza kukifanya hakuomba msaada wa ccm

Unatia aibu na kinyaa,ameongelea TAIFA lake hajakuongelea wewe.Kama huna cha kuandika ni bora kutokucomment ili uheshimike
 
Tundu Lisu ni retarded!
Ndiyo maana nimeanza kusema humu kumejaa misukule sikukosea na maana imeanza kujitokeza misukule niliyoisema. Unawezaje kumuita mtu aliyetoa wazo la maana kwa Taifa hili ni Retarded unless huielewi maana ya neno retarded.
 
Back
Top Bottom