figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, amenyimwa dhamana na atafikishwa mahakanai kesho.
Tundu Lissu alikamatwa na Polisi jana katika Viunga vya Bunge Dodoma na kusafirishwa kupelekwa Dar es Salaam Usiku usiku.
Mbunge Lissu amehojiwa kufuatia 'Press Conference' aliyoifanya Januari juu ya "Baa la njaa" akidaiwa kutumia maneno ya kichochezi.
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu (MB) baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi, amewekwa mahabusu ya polisi
Lissu ambaye hivi karibuni ametangaza nia ya kugombea kuwa RAIS WA CHAMA CHA WANASHERIA NCHINI (TLS) na kabla ya kukamatwa kwake alikuwa tayari ameshachukua na kujaza fomu ya kuwania nafasi hiyo, baada ya kuhojiwa kwa tuhuma za uchochezi, amebaki mahabusu kwa kile ambacho Jeshi la Polisi kupitia kwa ZCO Wambura, wamedai kuwa kuna mambo bado hawajakamilisha katika uchunguzi wao.
Mbunge Lissu anadaiwa kutoa maneno au lugha ya uchochezi Januari 4, mwaka huu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni, Dar es Salaam, katika mkutano ambao pia aliutumia kuzungumzia suala la Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kuhukumiwa kifungo cha miezi 6 jela.
Hii ni video ambayo alizungumzia njaa.
Mbowe aongea