Tundu Lissu: Afande Sirro na Kipilimba, Vijana wa Toyota Premio namba T460CQV Mliowatuma kunifuatilia nimewakaba

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878


Heshima kwenu Wakuu,

Leo Tundu Lissu ametoa ya Moyoni kwamba anawindwa na kufuatiliwa na vyombo vya Usalama. Amewasihi Vyombo vya Usalama vipambane na Wahalifu sio Wanaoikosoa Serikali

"Naomba kabla sijaanza Mazungumzo yangu nimuombe Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa anaitwa Kipilimba au Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro, wale vijana ambao wamewatuma na kwa wiki tatu mfululizo wananifuata kila nilipo wanaotembea na gari ya Toyota premio namba T460CQV, jana niliwakaba Kanisani St. Peter's.

Wakubwa hawa wa Vyombo vyetu vya Usalama wawaelekeze watumishi wao watumie muda na rasilimali za nchi hii wafanye kazi ya kupambana na Waharifu sio kupoteza muda wao na pesa zetu kuhangaika na raia ambao wanatimiza wajibu wao wa kuiwajibisha Serikali iliyoko Madarakani.

Kwahiyo Afande Sirro na Afande Kipilimba, fanyeni kazi ya kupambana na Wahalifu na tuachieni kazi ya kuwaajibisha walioko Madarakani kwa mjibu wa Sheria za Tanzania".
 
TISS wakufatilie kishamba hadi uwakabe? Duh! ....labda polisi wa kawaida wala si hata CID ....au labda ni wale wanaojiita Fichua uovu wa Shingongo ....big time joke ...hahaha ...eti nikawakaba ....dah
Hao itakua ni wapiga kura wake tu! Anasingizia watu wengine bure hapa kwa kutafuta sifa, ili tumuone eti naye ni bonge la mafia. Haha Lisu anaanza kutengeneza sinema za futuhi.
 
hivi unajua hata wewe wakiamua kukufutilia hawashindwi hawa watu! lisemwalo lipo,hahah ukiona hivyo ujue jamaa wanamlia timing, we unadhani kwa kauli zake watamuacha salama?

Ah wapi!

Hakuna anayeweza kunifuatilia mimi hapa bongo.

Wanaoweza kunifuatilia na wakafanikiwa ni IRS pekee.

Lakini siyo makachero uchwara wa bongo.

Wamfuatilie kwa minajili gani?

He is delusional.
 
Back
Top Bottom