Elia F Michael
Member
- Mar 3, 2018
- 75
- 800
Juzi nimepokea taarifa kutoka kwa Diwani Mwenzangu Hapa Kakonko kuwa kuna watoto 2 walifariki kwa kuangukiwa na kipande cha ukuni uliodondoka kutoka juu ya mti wa Mrumba,mti ambao unatumiwa kama darasa la kujifunzia, kwa lugha rahisi wamefariki wakiwa Darasani.
Najua hawajafariki kwa mapenzi yao,ila wamefariki kutokana na umasikini wa nchi yetu ambayo haina uwezo wa kujenga madarasa huku ikijinasibu kutoa elimu bure. Ni kweli kuna elimu bure ndio maana wanasomea chini ya Mrumba na wakidondokewa na kuni wakafa taarifa zao zinafukiwa na hazijulikani kama ni matukio magumu na ya kushitua. Kwa hili sitashangaa sana maana Kakonko nayo ipo pembeni sana mwa nchi hii ya elimu bure isiyo na madarasa ya kutosha wala nyumba za walimu.
Kama ilivyo ada hawa nao wapumzike mahala pema peponi maana hakuna namna,tumewaua tena kifo kibaya,kifo cha kudondokewa na kuni huku wakiwa chini ya mti wa Mrumba ambao ndilo darasa lao ambalo elimu bure inatolewa.
Mimi pia kwenye Kata yangu kuna watoto ambao wameanza shule lakini wanaishi mazingira magumu sana.
Wanaishi kilomita zaidi ya 40 kutoka makao makuu ya kijiji,wamezaliwa kwa wananchi ambao ni wakulima ambao walienda porini kutafuta ardhi yenye rutuba baada ya ardhi ya nyumbani kijijini Nyakiyobe kupungukiwa rutuba.
Huko wamefika wakaendeleza uzazi,mpaka mwak2015 hakuna aliyekuwa anasoma huko.
Nilipoingia kama Diwani,tulijitahidi na wananchi kuezeka kwa bati vyumba viwili lakini sasa vyumba hivyo vimejaa na sasa wananchi wamewajengea kuta za miti na udongo ili zitumike kama Darasa ili nao waweze kupata elimu bure.
Wengi wanakalia magogo ya miti na wengine chini kwenye udongo.
Mvua inaponyesha chumba hicho hakikaliki,pindi wanaporudi nyumbani mchana wa jua kali na wanapita porini,wengi wanakimbizwa na nyoka aina ya koboko.
Tayari tumeshawazika watoto 3 kwa kudonolewa na nyoka aina ya koboko,hivi ni vifo vya kawaida saana kwenye mazingira haya ya pori.
Unaposimama kulisemea jambo hili kwenye vikao,unaambiwa uhamie CCM. Tena dau kubwa linatangazwa ili wanase tu saini yako. Inawezekana kabisa wao hawajui haya maeneo,maana magari yao hayawezi kufika huku ndio maana hawajali utu wa watu!
Hivi Ukuu wa Wilaya ama Ukuu wa Mkoa ama Kujiuzulu udiwani ili uchaguzi urudiwe Gwarama ndio utafanya maisha ya watoto 2 waliodondokewa na ukuni wakafa wapate uhai warudi shule? Ama wale 3 waliodonolewa na nyoka warudi kwenye uhai wao? Ama hawa waliokalia vipande vya miti wapate madawati?
Nikisema serikali hii haijali utu wa mtu nitakuwa ninakosea?
Nilikuwa nimemngoja Waziri mkuu kwa hamu sana hapa Kakonko kwenye ziara yake sasa naona ameahirisha Mara ya 4!
Sasa naanza kuamini kwamba yule Mkurugenzi wa Kakonko Ndugu Lusubilo Mwakabibi ambae aliiba fedha za OC ya mwezi Decemba 2017 Tsh 36,904,000.00 na hakufanywa kitu kweli ana mahusiano na Bwana Kassim Majaliwa.
Huku kwetu mpunga huo umepigwa,ili kupoteza ushahidi Mhasibu wa Wilaya(DT) amehama,Mkaguzi wa hesabu amehama,afisa mipango amehama,mwanasheria amehama,afisa utumishi amehama na Mkurugenzi mwenyewe amehama. Sisi tumebaki na hoja za ukaguzi zisizo na majibu. Sasa nilitaka huyu Mh Waziri Mkuu aje atueleze huu utaratibu ni wawapi wa kuhama kikosi chote hiki ndani ya muda unaofanana!
Hii serikali inaonekana Matatizo yakitajwa na viongozi wanaotokana na upinzani yenyewe haitambui kama ni matatizo, Ukiacha hayo maafa ya MV Nyerere yaliyoua kijiji kizima lakini bado wakubwa wanaona wanafaa kuwa ofisini mpaka leo,bado ninaona utu wa watu unazidi kupungua kila Leo.
Huku kwetu mtumishi akifa akiwa kazini anazikwa ndani ya jeneza la Mabanzi na Mkurugenzi huyu Bwana Lusubilo Mwakabibi yeye hakuwa na utamaduni wa kutuma muwakilishi wake. Mwalimu wangu mmoja ambae alifariki mapema mwaka huu tar 04/01/2018 , Mwalimu Peter kiyuzi Kineye yeye pia alizikwa ndani ya mabanzi nikiwa naona na kwa bahati Mbaya Mkurugenzi hakutuma muwakilishi wake.
Sasa kituko kingine ni cha Mkuu wa shule ya sekondari Kakonko ambaye alijinyonga tar 26/03/2018 kwa kuacha ujumbe ya kwamba"Mkurugenzi wa Kakonko asipodhibitiwa ataua wengi" yeye angalau Mkurugenzi alilipia jeneza la mabanzi ila sasa wakati wa utengenezaji wa jeneza hilo marehemu hakupimwa urefu ila walikadiria vipimo na wakati wa kuweka mwili wake haukuenea ikabidi washindilie ili asafirishwe kwenda Mwanza. Aibu tupu zikawajaa waombolezaji wakaamua kununua jeneza pale Katoro.
Mh Waziri Mkuu,Ukipanga tena kuja Kakonko usiahirishe maana tuliyofanyiwa na Mkurugenzi huyu wa TEMEKE hatutayasahau. Nasisitiza kwamba Bwana huyo ni mwizi na Mkiendelea kumlinda mtawaumiza sana wananchi.
Mwisho,napenda kuendelea kuwashukuru wadau hawa wa EQUIP ambao wanaendelea kusaidia madarasa shikizi haya ambayo serikali yenyewe inaona vipaumbele vyake ni viwanda ambavyo havitegemei sekta ya elimu kuboreshwa sana.
Niishauri serikali hii hata kama haisikii ijikite kwenye elimu kwanza maana hata mataifa makubwa duniani kama Uingereza iliwachukua miaka zaidi ya 100 kufanya mabadiliko kwenye viwanda lakini walianza na elimu,baadae kilimo na baadae viwanda!!!
Karibuni KAKONKO.
Elia F Michael.
Diwani Gwarama.
Mbunge nje ya Bunge.
Mwenyekiti wa madiwani Kanda ya Magharibi.
04/October/ 2018.
Nzega-Tanzania.
View attachment 885318