Hatuna muelekeo. Tupo tupo tu. Wenye kuona wameshaona na ahadi nyingi za ajabu na nyingine kushindikana kwa kasi;
- Hivi ile bei ya Sukari tuliyoahidiwa ndio hii ya sasa? Mbona inapanda? Au ndio kuongeza makusanyo ya kodi?
- Usafi nao uliishia wapi? Mbona Jiji ndio linazidi kuchafuka. Masoko ni machafu haswaa na kipindupindu kitaibuka muda si mrefu.
- Nini tathmini ya elimu bure? Mbona hatuzungumzi namna michango inavyorudi kwa mlango wa nyuma. Ilikuwa ni haraka au sifa?
- Toka tumejivika weledi wa utumbuzi, nani ameadhibiwa? Hapa nimgusie Mh Kilango. Mama yule wakati wenzake wamekazana kuifilisi nchi aliwahi kuinuka na kupiga kelele, wananchi wanaibiwa. Leo hii kadanganyika, basi akawa mdhalilishwaji wa hali ya juu. Tukikosea hakuna onyo? Ukipewa kazi ya udereva, ukigonga tu hata kama ni kwa sababu ya ubovu wa chombo wewe ni kunyang'anywa leseni na hutoendesha gari tena. Kwani hakuweza kurekebishika mama yule?