Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,188
- 1,604
Ni nani ambaye hajui kuwa ccm inapita katika bonde la uvuli wa mauti! Naaam, ni mahali hapa ambapo vyama tawala barani africa hufika na kufutika katika ramani za siasa.
Pamoja na kuwa natamani ccm ishindwe kabisa katika uchagizi huu, lakini sipendi taasisi hii kongwe ife kifo cha mende. Ni kwanini nataka ccm itoke magogoni lakini isiondoke Lumumba na dodoma?
Tusijidanganye wenyewe, maana ili tupige hatua za maendeleo tunahitaji chama tawala imara, na upinzani imara pia. Ndio maana kwa upande mmoja nafsi yangu inawapongeza sana mashujaa wanaotoka ccm na kujiunga katika kambi ya ukombozi, ingawa upande mwingine nakuwa na wasiwasi iwapo chama hiki kitasalimika hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi unaotukabili.
Pengine unaweza kujiuliza swali, kwanini mambo haya mara nyingi hutokea zaidi afrika na si kwingineko
Tatizo ni kwamba vyama tawala barani havina msamiati wa kushindwa, na kwa hivyo huwa hawajajipanga kwa ajili ya hilo. Sasa basi lile lisilopendwa linapotokea; wanasiasa hao hustushwa mithiri ya mainzi yaondokavyo kwenye mashonde.
CCM mmechafuka, ni kweli, hamtufai sasa. Lakini hali hii haitaendelea siku zote. Mkibadilika ninyi na sisi tutabadikika nakuwahitaji tena. Kubalini kupata uzoefu ambao hamna sasa! Ninamaanisha uzoefu wa upinzani. Chonde chonde jamani, muungwana akivuliwa nguo huchuchumaa.