Tunasubiri Mkuu wa Nchi Akachome Mashamba ya Bangi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mkuu wa nchi alipotua jana kutoka Uganda akaanzia uwanja mdogo wa ndege katika eneo la kufikia wageni, ukisikia yale mahojiano aliyofanya na wale wafanyakazi unaona kabisa kuwa 'Mwenye Nchi Karudi'. Nilikuwa mahali na vijana wengi sana na ungelimsikia kila kijana akisema "Naam, nchi imepata mwarobaini!".

Jambo lile likanifanya nitafakari upya kujua kama tumepiga hatua, nikagundua bado tunapiga MARK TIME! Pamoja na mikakati yote ya Rais na hatua zote anazochukua na kutumbua kote anakotumbua na kufukuza kote anakofukuza, bado kila anakoenda yeye mwenyewe unakuta watendaji wamelala usingizi wa PONO, FOFOFO!

Kwa kweli jana nimejisikia vibaya sana na nikamhurumia sana JPM! Je mamlaka ya viwanja vya ndege haiko chini ya wizara? Wizara haina waziri, Makatibu wakuu, makatibu wakuu wasaidizi, wakurugenzi na maofisa wa kila aina? Wote hawa walikuwa wanapita tu pale uwanja wa ndege bila kuchukua hatua yoyote hadi rais afike! Rais atafika wapi na wapi kabla miaka mitano haijaisha my poor country Tanzania!

Kwamba vijana wanabeba matumaini makubwa, kwamba nchi imepata mtu imara sana, ndiyo - imara sana na ambaye hana masihara! Lakini mlijifunza nini jana mlipoona kila mfanyakazi anayekuja anamdanganya rais, hadharani, bila hofu wala soni - bila kupepesa macho.

Wanadamu wa karne hii siyo waoga kama tunavyodhani, na kama watu waliidhani STYLE ya JPM ya kuzunguka huku na kule kwa kushtukiza itaibadilisha nchi hii kwa miaka 5 au 10, wafanye utafiti mpya. Na kama watu walidhani STYLE ya JPM itawaogopesha watumishi wa umma, wakafanye utafiti upya.

Kama JPM na wenzake hawatafumua mifumo yote ya nchi na kuifanya ianze kazi upya kupitia KATIBA na SHERIA rafiki, za kisasa - hatuendi kokote. Kama JPM na wenzake hawatawekeza nguvu za maamuzi na utendaji kazi unaojipima katika taasisi moja moja ya serikali, hatuendi kokote.

Sasa tutageuka kuwa nchi ambayo usalama wa Taifa wakihisi kuna bangi imelimwa kule Iringa na RPC hajachukua hatua, wanakuja kum-TIP JPM na siku akiwa na ziara Iringa ndiyo anakwenda mwenyewe kuchoma bangi hiyo.

Tumeendelea kuwa taifa la ajabu sana linaloamini kuwa nchi hii itabadilishwa na mtu mmoja! Bahati nzuri mtu huyo imara tunaye hivi sasa, count on me in five years ndiyo utakubaliana na kauli ya Barack Obama, kwamba "Africa does not need strong men, it needs strong institutions".

Kuweni na wikendi njema.

Mtatiro J
 
Magufuli ataibadili hii nchi peke yake .. tatizo hakuna kiongozi mwingine yoyote anayeaminika na Watanzania wengi Zaidi ya rais...na anajua kutenda wananchi wanayoyataka.....wanasiasa poleni sana wananchi wameshapoteza Imani kabisa na wanasiasa Imani yao iko kwa rais tu...
 
Si mlisema kiongozi legelege huzaa serikali legelege, kwa vile mmeona jpm yu imara mnaanza kutapatapa, mue mna recall nyuma mlisemaje kwanza ndio mfikirie mambo wa kuandika, muwe na msimamo
 
Kwa tukio la Uwanja wa Ndege kwa kiongoz makin kama Aliyekuwa rais wa Zambia Marehem Michael satta, Pale angemtumbua Wazr husika,. Tatizo la Magu anataka amtumbue mpaka mfagizi wa Ofc
 
This time mtanyooka tu, mlizoea business as usual. Ni lazima mbadilishe mitazamo ya kivivu ili muweze kuendana na muziki wa JPM. Na hizo lawama na manung'uniko yenu wala haziwezi kuwasaidieni. Mtakuwa mnabadilisha magoli kila kukicha.
 
Back
Top Bottom