Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Tunarudi Tena Mwezini. Picha unayiona ni Alama ya mguu baada ya binadamu kutua Mwezini ๐ฅพ.
Imepita zaidi ya Miaka 56, baada wanaanga Toka Nasa Neil Armstrong na Buzz Aldrin walipofika Mwezini, na kuwa wanadamu wa kwanza kutembea kwenye Ardhi ya mwezini. Sasa wanafanya kazi Tena ya kurudi Mwezini.
Sio stori Tena ni kitu cha ukweli, NASA wataweza kushirikiana na washirika wa kimataifa na kibiashara ili kurejea Mwezini Kisha kukaa kwa muda mrefu huko , ambapo mchakato huo ni hatua muhimu katika kuelekea kwenye Sayari ya Mars.
Sayari yao itaweza kusaidia kuweza kufanya tafiti Mbalimbali za kisayansi na Teknolojia ambapo lengo lao ni kuwezesha wanadamu kusafiri na kutalii mbali na Dunia.
NASA imesema " tunataka kujifunza kuhusu sayari Nyekundu kuhusu mambo ya kale na yajayo ya Dunia huenda itasaidia kujibu ikiwa kuna uhai zaidi ya sayari yetu ya nyumbani.