Tunaona hapa, mabepari wanaona kule

MKILINDI

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
732
948
Watanzania tunafurahika sana na yanayotokea kwenye sakata la madini na makinikia ya mchanga. tena tunafarijika kuona tumemtoa nyoka pangoni kwa kumtoa C.E.O wa barrick, canada na kuja kufanya majadiliano bila kuitwa.

Ila inasikitisha sintofahamu ya taarifa ya kukubaliana kulipa baada ya mazungumzo alikadharika hapohapo kuna barua ya kampuni inayokana kufikia mahitimisho ya kuilipa Tanzania tangu 1998 ila inakubaliana kuwa kweli C.E.O wao kuja na kufanya mazungumzo na Rais.

Kwa historia ya nchi nyingi za dunia ya tatu hasa hizi za Afrika. misukosuko ya vita ya kiuchumi kama hii na mabepari wakubwa ambao sio interest ya nchi moja kama wanavyoonekana katika bodi yao. ni wazi kuwa vita hii si ya kitoto kama tunavyowaza na kufurahia kwa muda.

Wengi wetu ( AFRIKA ) tunaona hapa. tunaona kulipwa ili kutimiza haja zetu za muda mfupi. lakini wenzetu wanaona mbali na kutimiza malengo yao ya muda mrefu hata kama yeye hatokuwepo basi kitukuu chake kitafurahia matunda yake.

Ninachoamini ni kuwa wakati sisi tukisubiri mabepari watasemaje kuhusu hili. wao hawalali wanafanya vikao usiku na mchana kuweza kutoka katika hili kwa namna yoyote ile.

Nikiitafakari Siera Leone na blood diamond moyo unanidunda.. Congo na vikundi vya waasi napata kizunguzungu nk mifano ipo mingi kwa nchi nyingi za afrika zenye machfuko kwa ajili ya madini. simaanishi kuwa tusidai chetu kwa kuogopa hayo. La hasha isipokuwa jibu watakalotoka nalo baada ya vikao vyao vya usiku kwa usiku.

NAWAZA MAWAZO YAO. NJIA WANAZOWAZA ILI KUPATA JIBU LA KUDUMU.
wanaanza na maswali haya:
  • Kwanin limetokea mwaka huu 2017 wakati chama ni kilekile?
  • Wametengemaa kiuchumi kiasi gani? vipi tukiweka vikwazo kama zimbabwe, wataendelea?
  • Vipi tabia zao..wanaomba sana misaada kama wale waliopita?
  • Waliopo wanatabia kama za waliopita? hawasafiri safiri tummalizie hukuhuku ughaibuni?
  • Kama akiondoka yule wa juu, atatokea mwingine?
  • Vipi kuna chama cha siasa chenye kutamani madaraka nchini mwao?
  • Rafiki wao mkubwa kisiasa ni nchi gani?
  • Vip hamna machafuko katika nchi zinazozunguka
MAJIBU YA MASWALI HAYO YANALETA HATUA ZA KUCHUKUA
  • Tumtume boss kwanza tuone hitaji lao hasa ni lipi
NB; niliyoandika ni mawazo tu, ambayo anayependa kufikirisha fikra zake hulazimika kufikiri hivyo haishii kusema. WATANZANIA TUUNGANE KWNY VITA HII YA KIUCHUMI.
Kwa deep thinkers na reasoning person ndiye pekee atakayeona kuwa nilichoandika kina uzito wa kiasi gani katika kupata majibu yao ya kudumu.
jibu lolote hapo juu la YES au NO lenye interest kwao linaweza kutengeneza mpango wa miaka 7 ya majaribio.

kwa leo naandika machache..tafuta majibu yenye interest zaidi kwao ili uzidi kujiweka salama. zaidi ya kufikiria kulipwa pesa ukajisahau wakatengeneza mipango kama ya russia ya Goberchev.

BY
F.B.I WA MORO.
 
umeandika vizuri ila mwisho umeharibu kwa kulazimisha wote tukubali mtazamo wako..lakini ahasante kwa kutoa angalizo,watu wa usalama watalifanyia kazi.

Sina nguvu ya kukufanya uwaze nzchowaza. nawaza najikuta nawaza extra miles kwa kile nnachoamini katika figisufigisu za mabepali.
 
Akili ndogo. ..unalazimisha toune kuwa tutaishia kwenye vita no way ukiwa bold hata wao wananywea ...
 
Alarm ilitakiwa ilie pale ambapo mwenyekiti wa Barrick alipoambatana na Balozi wa Canada hapa nchini. Ikumbukwe Canada ni mdau mkubwa wa mikopo/misaada ya kibajeti. Sasa misaada na mikopo ina masharti sana. Tutegemee Barrick 'kujitakasa' na Canada 'kuilazimisha' serikali ikubaliane na Barrick kwa kutumia misaada.

Let's not rejoice for winning a battle, there is fierce war ahead.
 
well said
 
Akili ndogo. ..unalazimisha toune kuwa tutaishia kwenye vita no way ukiwa bold hata wao wananywea ...
ndipo ulipoishia kufikiri. soma kwa makini nnachokiandoka hakuna sehemu nnayosema tutapigana vita.
kuna masulihisho mengi yanayopatikana kutokana na maswali adidu hapo juu.
  • Yaweza kuwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.
  • kupandikiza mtu wao.
  • assasnatioN
  • NK
BADO KIJANA. THINK BIG ACHA VITAMBO.
 
NB; niliyoandika ni mawazo tu, ambayo anayependa kufikirisha fikra zake hulazimika kufikiri hivyo haishii kusema. WATANZANIA TUUNGANE KWNY VITA HII YA KIUCHUMI.
Kwa deep thinkers na reasoning person ndiye pekee atakayeona kuwa nilichoandika kina uzito wa kiasi gani katika kupata majibu yao ya kudumu.
jibu lolote hapo juu la YES au NO lenye interest kwao linaweza kutengeneza mpango wa miaka 7 ya majaribio.

kwa leo naandika machache..tafuta majibu yenye interest zaidi kwao ili uzidi kujiweka salama. zaidi ya kufikiria kulipwa pesa ukajisahau wakatengeneza mipango kama ya russia ya Goberchev.

BY
F.B.I WA MORO.

Hakuna vita ya uchumi hapo, kwani Barick walikuja na vifaru kutulazimisha kuchukua madini?, Mafisadi yetu Chenge and Co ndio wametufikisha hapa
 
Mi nadhani hata magufuli anaujua ugumu wa anachokifanya, au hajui? Ukijibu ndio uniambie pia kama unafanya kazi ikulu.
 
Watanzania tunafurahika sana na yanayotokea kwenye sakata la madini na makinikia ya mchanga. tena tunafarijika kuona tumemtoa nyoka pangoni kwa kumtoa C.E.O wa barrick, canada na kuja kufanya majadiliano bila kuitwa.

Ila inasikitisha sintofahamu ya taarifa ya kukubaliana kulipa baada ya mazungumzo alikadharika hapohapo kuna barua ya kampuni inayokana kufikia mahitimisho ya kuilipa Tanzania tangu 1998 ila inakubaliana kuwa kweli C.E.O wao kuja na kufanya mazungumzo na Rais.

Kwa historia ya nchi nyingi za dunia ya tatu hasa hizi za Afrika. misukosuko ya vita ya kiuchumi kama hii na mabepari wakubwa ambao sio interest ya nchi moja kama wanavyoonekana katika bodi yao. ni wazi kuwa vita hii si ya kitoto kama tunavyowaza na kufurahia kwa muda.

Wengi wetu ( AFRIKA ) tunaona hapa. tunaona kulipwa ili kutimiza haja zetu za muda mfupi. lakini wenzetu wanaona mbali na kutimiza malengo yao ya muda mrefu hata kama yeye hatokuwepo basi kitukuu chake kitafurahia matunda yake.

Ninachoamini ni kuwa wakati sisi tukisubiri mabepari watasemaje kuhusu hili. wao hawalali wanafanya vikao usiku na mchana kuweza kutoka katika hili kwa namna yoyote ile.

Nikiitafakari Siera Leone na blood diamond moyo unanidunda.. Congo na vikundi vya waasi napata kizunguzungu nk mifano ipo mingi kwa nchi nyingi za afrika zenye machfuko kwa ajili ya madini. simaanishi kuwa tusidai chetu kwa kuogopa hayo. La hasha isipokuwa jibu watakalotoka nalo baada ya vikao vyao vya usiku kwa usiku.

NAWAZA MAWAZO YAO. NJIA WANAZOWAZA ILI KUPATA JIBU LA KUDUMU.
wanaanza na maswali haya:
  • Kwanin limetokea mwaka huu 2017 wakati chama ni kilekile?
  • Wametengemaa kiuchumi kiasi gani? vipi tukiweka vikwazo kama zimbabwe, wataendelea?
  • Vipi tabia zao..wanaomba sana misaada kama wale waliopita?
  • Waliopo wanatabia kama za waliopita? hawasafiri safiri tummalizie hukuhuku ughaibuni?
  • Kama akiondoka yule wa juu, atatokea mwingine?
  • Vipi kuna chama cha siasa chenye kutamani madaraka nchini mwao?
  • Rafiki wao mkubwa kisiasa ni nchi gani?
  • Vip hamna machafuko katika nchi zinazozunguka
MAJIBU YA MASWALI HAYO YANALETA HATUA ZA KUCHUKUA
  • Tumtume boss kwanza tuone hitaji lao hasa ni lipi
NB; niliyoandika ni mawazo tu, ambayo anayependa kufikirisha fikra zake hulazimika kufikiri hivyo haishii kusema. WATANZANIA TUUNGANE KWNY VITA HII YA KIUCHUMI.
Kwa deep thinkers na reasoning person ndiye pekee atakayeona kuwa nilichoandika kina uzito wa kiasi gani katika kupata majibu yao ya kudumu.
jibu lolote hapo juu la YES au NO lenye interest kwao linaweza kutengeneza mpango wa miaka 7 ya majaribio.

kwa leo naandika machache..tafuta majibu yenye interest zaidi kwao ili uzidi kujiweka salama. zaidi ya kufikiria kulipwa pesa ukajisahau wakatengeneza mipango kama ya russia ya Goberchev.

BY
F.B.I WA MORO.
Tutakuwa na bahati ya ajabu sana tusipopigana vita na malawi.
Ni vita ya kiuchumi.
 
Hakuna vita ya uchumi hapo, kwani Barick walikuja na vifaru kutulazimisha kuchukua madini?, Mafisadi yetu Chenge and Co ndio wametufikisha hapa
Kikwete ndiye alisaini, usimsingizie chenge.
 
Hii vita imekuja wakati tete. Taifa lolote kiuchumi ni imara pia kijeshi. Je ni kipi kinatakiwa kianze kati ya kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama au kuimarisha uchumi?
Ukiwa na rasilimali bila ulinzi kunaweza kutokea machafuko yanayo chagizwa na wananchi wenyewe kwa kugombea rasilimali husika au mataifa ya nje yakafanya "foju" ili nchi isitawalike na WAO kuweza kujichotea Mali watakavyo.
Wananchi wa kawaida, wasomi, wanasiasa na wataalamu wa ulinzi na usalama, tuamke tuitete na kuilinda nchi yetu.
 
Back
Top Bottom