Acha Uvivu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 524
- 131
Haina ubishi kwamba wazanzibar siku zote wako mbele kuliko watu wa bara, wanajielewa na wanajitambua. Kwao utaifa ni jambo la kwanza kuliko chama, hasa kwa wenye maono waliyo ndani ya CCM kutotishika na siasa za maslahi na ufisadi wa chama hicho kikongwe lakini kichanga kuliko busara za akina mzee Moyo.
Wakati wazee wa CCM bara, wakitishiwa nyau hawako tayari kujitoa mhanga mpaka hatua ya kufukuzwa mapema wanakuwa tayari wameshalainika na kurudi katika kundi la maadui waliyodai kuwapinga.
Hoja pekee, ni kuwa kwa uoga wa watu wa bara na kukosa msimamo imepelekea wazanzibari kulaumu wabara kama kikwazo pekee cha ukombozi wa pili visiwani. Kweli hili halina ubishi, ukirejea ushindi wa CUF visiwani katika chaguzi 3 mfululizo lakini ushindi ukibatilishwa kwa nguvu ya wana CCM wa bara ambao wamekuwa wakitegemea uoga wa watanganyika kujidhatiti.
Sasa kuna watu hawa, Mansour Yusufu na Mzee Moyo ambao hawajataka kuburuzwa. MANSOUR amejiunga CUF na Mzee Moyo akiwa mstari wa mbele kuwaelimisha wazanzibar hasa kuhusu Muungano kama ilivyopendekezwa katika Katiba chini ya Mzee Warioba.
Sasa ningeshauri hawa wazee wavuke bahari kuja bara, wasaidiane na UKAWA na kuifuta kabisa CCM.