Katika pitapita yangu vijiweni maofisini na sehemu mbalimbali kuna baadhi ya watu wanalaumu utendaji wa Rais Magufuli na wengine sasa kusingizia kila kitu Magufuli.
Mimi binafsi kwa akili ndogo tu ukiwasikiliza hawa wanaolalamika hawana hoja.
1. Mfano kulalamika kuwa ofisini kimefutwa kila kitu ni uongo. Hili linasababishwa na viongozi wengi wa nchi hii huko maofisini kuwa waoga kupita kiasi. Badala ya kufanya kazi kwa weledi wao na kusimamia baadhi ya mambo wamekuwa wakiishia kusema rais kasema rais kasema kitu ambacho sio kweli. Mfano sijasikia rais anasema futeni chai ofisini, futeni allowance mtu akifanya muda wa ziada na mengine mengi.
2. Matumizi. Suala la matumizi ni kweli rais amesema tubane matumizi lakini pale ambapo inahitajika kutumika na ukajenga hoja hamna zuio ila kwa uoga wa viongozi wetu na watu weusi tulivyo wanafiki utasikia utatumbuliwa siipitishi hiyo hela ya kazi zako.
3. Maisha mtaani hii imewakumba wengi. Tulizoea kupiga deal za haraka haraka lakini kama unafanya kazi zako za halali hela utapata hata kama ni kidogo tena nchi yetu nzuri sana tembelea nchi jirani uone maisha yalivyo. Tuache kubeza kila kitu.
4. Unafiki wa watanzania. Watanzania wengi ni wanafiki sana....wakati JK yupo madarakani aliitwa majina lukuki na kila mtanzania alishoboka leo Magufuli anafanya tofauti na JK naye wameenza kumuona na kumsema kila aina ya maneno...watanzania tubadilike. Badala ya kufanya kazi kwa bidii na kuhangaikia maisha yetu muda wote watu wako kujadili rais hafai, oh hataweza sisi kila kitu ni kulalamika na kubezana tu
5. Mwisho Viongozi walioko maofisini wabadilike wafanye kazi kwa kanuni na sheria zilizopo. Sidhani kama Magufuli yupo tayari kuona watanzania wenzake wananyimwa haki zao za msingi kama tunatumia bajeti zetu kwa usahihi bila uoga na unafiki.
Nawasilisha.