Tunajenga kizazi gani?

Mambo engine tunajitakia wenyewe kwa kushadidia. tamaduni za Magharibi na kuacha za kwetu Waafrika.
Mfano tumekuwa tukitumia nguvu Sana kupinga adhabu ya fimbo mashuleni na majumbani,matokeo yake tunakuja kutumia risasi na magereza kuwarekebisha watu wakishakuwa wakubwa.
Tumekuwa pia tunatumia nguvu nyingi kutaka 50 Kwa 50 na usawa Kati ya wanaume na wanawake,matokeo yake tunashangaa kuona ndoa nyingi zinavunjika na kuathiri malezi ya watoto.
Mifano ni mingi,Itoshe kusema tu kwamba tunatakiwa tujitathmini kama Taiga ili tuachane na Tania ya kudandia tamaduni na Mila za kigeni kwa kisingizio cha Utandawazi.
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa sana na hapa kusema ukweli ni tumeshindwa kujisimamia na tumekubali kuishi kama nguruweโ€ฆ
 
Hawa wazazi wa sasa wanaoonekana kuwa wa hovyo si ndio walilelewa na hao wazazi wa zamani.
Sasa hawa wazazi wa sasa hiyo tabia ya kukosa uvumilivu wamejifunzia wapi kama wazazi wao hawakuwa na hiyo tabia?
 
Shida yangu ni moja, kila Bar Maid niliyeongea naye mahali popote ni Single Maza, sijawahi kujua hii connection
 
Zamani, wazazi wetu walikuwa wanaishi kwenye jamii ndogo. Changamoto za ndani ya nyumba walikuwa wanazijua wao wawili au na ndugu wa karibu sana. Hakukuwa na mtu wa kuwaambia kuwa maisha yao ni mabaya. Siku hizi, kijana akiamka tu asubuhi, anafungua Instagram au TikTok na kukutana na mamilioni ya watu wanaorusha maisha yao ya uongo na kweli ya kifahari.

Hapa ndipo ugonjwa unapoanzia. Unaanza kuona mbona mume wa fulani anampa zawadi kila wiki, mbona mke wa fulani hapigi kelele? Huu ulinganishaji huwa unaleta kile tunaita FOMO. Wazazi wa zamani hawakuwa na hii presha ya kidunia, nyinyi vijana wa kisasa mmebatizwa na mawazo ya nje yanayowaambia you deserve better kila mda, hata kwa mambo madogo sana ya kijinga.
 
Unataka kuniambia hata hawa wazazi wa miaka 36 na kuendelea hadi 50 nao wanaendesha maisha yao kwa pressure za mitandao ya kijamii?
Kama jibu lako ni ndiyo, tafsiri yake inaweza kuwa hawajakomaa kiakili na kihisia au kama jibu ni hapana wanaweza kuwa na changamoto nyingine za tofauti ambazo jamii haijaamua kukaa chini na kuzifanyia kazi.

NB
Miaka ya 90 ambako hakukuwa na mambo ya mitandao ya kijamii niliwahi kushuhudia wanandoa kadhaa wakivunja ndoo zao. Hao nao utasema walikuwa na FOMO?
 
Unataka kuniambia hata hawa wazazi wa miaka 36 na kuendelea hadi 50 nao wanaendesha maisha yao kwa pressure za mitandao ya kijamii?
Jibu ni ndio kwa sababu kwenye ukuaji wao hakukuwa na interaction kubwa ya mitandao ya kijamii ukilinganisha na sasa.
Miaka ya 90 ambako hakukuwa na mambo ya mitandao ya kijamii niliwahi kushuhudia wanandoa kadhaa wakivunja ndoo zao. Hao nao utasema walikuwa na FOMO?
Zilivunjika yes lakini sababu ya kuvunjika ni tofauti sana na hizi ndoa za sasa na ndiyo msingi wa mada hii.
 
Shida yangu ni moja, kila Bar Maid niliyeongea naye mahali popote ni Single Maza, sijawahi kujua hii connection
Anaamini Bar ndio kitegeauchumi baada ya kuachika kwenye ndoa,isitoshe wengine wanazaa kama burudani hivyo mzazi mwenza hayupo kwenye muhimili wake ndio mana inatokea wanaamua kwenda kuuza pombe na nyuchi.
 
Kwa hiyo wanaacha Ndoa kwa lengo la kuwa huru kuuza nyuchi?
 
Unacho kisema ni kweli mkuu,wazazi wa wazamani hawakuwa na katabia ka tamaa hata kidogo,na walishirikiana kinagaubaga na wenza wao kitimiza haja.
 
Kwa hiyo wanaacha Ndoa kwa lengo la kuwa huru kuuza nyuchi?
Hiyo Biashara huenda ikawa ya kuibiaakini ikitokea unakutana na mwanamke anauza bar ni kitu gani kinakujia kichwani mwako๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ