Bila demokrasia makini huwezi kujenga mfumo madhubuti. JPM anaweza akawa anataka kushughulikia ufisadi, ulege lege kazini n.k lakini bila demokrasia inayoleta checks na balances ataondoka na kila kitu chake akija mwingine tutaanza tena. Tuna watawala wenye nguvu sana kikatiba ambayo huwapa uhuru wa kufanya wapendacho hata kuwa madikiteta (hili kalisema si mwingine bali Julius Nyerere mwenyewe), tuna uchama dola (nguvu ya CCM inatokana na hili zaidi - Zanzibar ni mfano, na Tanganyika tunalijua na kuli-ishi), kulindana (mwenyewe anasema hata fukua makaburi, hata na yeye akimaliza kusiwe na wa kumhusisha na chochote alichotenda kabla na baada ya kuwa raisi). Mpaka tutakapo pata dawa ya haya mafanikio yote atakayopata yataondoka na yeye. Na haya matatu ni mambo ya kikatiba na kuiishi hiyo katiba-yeye anasema haikuwa kwenye ilani yake hivyo kwa sasa si kipaumbele chake. Kama kweli anataka legacy yake-ajenge mfumo imara-lazima ashughulikie hayo.