Tunahitaji mfumo imara,JPM chukua hatua!

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
2,000
Bila shaka mh JPM amethubutu katika kushughulikia changamoto za ufisadi japo kuna "lose ends" nyingi!Tunakubaliana wote kuwa siku moja JPM hatakuwa Rais,na hii inaweza tokana na sababu kuu 4:
1.Kutochaguliwa 2020
2.Kukaa kando ya ulingo kikatiba 2025
3.Maradho\kifo(Mungu epushia mbali)
4.Nyinginezo kama kujiuzulu nk

Je,utapenda kuona yale uliyopambana nayo yakirejea???
Utawala huu wa JPM umenifunza kuwa katika nchi yetu,mambo makubwa na nyeti yanategemea maamuzi ya Rais au watu wanavyomtafsiri!Ndio maana pamoja na kashfa zote zilizowahi kutokea huko nyuma ilikuwa ni kama mambo ya kawaida tu!Ilifika kipindi mpaka nchi za watu wanatusaidia kuona kuwa tunaibiwa,refer sakata la radar!Lakini ndio kwanza sisi tulikuwa tunavuta shuka,mpaka wanaturudishia chenji wala hatuna habari!
Kuna guarantee gani kwamba hatutarejea huko?Umechukua hatua gani ili basi hata Rais anapokuwa dhaifu basi nchi hailipi gharama kwa udhaifu wake?Je,kuna mfumo unafikiria kuuweka ili basi hata Rais anaposema "pesa sio za umma" isiwe end of the story???
Au unataka upate credit tu kwa kipindi chako ,the rest tutajijua mbele ya safari?
Nakusihi sana uunde mfumo ambao hautarely sehemu moja katika kuresolve national issues!
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,520
2,000
viongozi wa afrika ni ngumu kujenga mifumo huru kamwe. labda mifumo yao binafsi na sio ya kitaasisi. jpm hawezi kutoka nje ya kundi hilo kamwe.
 
Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
3,926
2,000
Asimsahau na yule aliuza nyumba za serikali pamoja na kununua kivuko kibovu Ikibidi amnyonge kbsa.
Teh teh teh
...dikiteta uchwara ndiyo nani? Nasikia watu wanamsema......
 
Erastojhn

Member
Apr 1, 2012
66
125
Viongozi wa Africa hasa hapa kwetu hawaamini ktk kujenga taasisi zenye nguvu na katiba yenye sauti na itokanayo na wananchi,maana wanaamini wao wana akili nyingi kuliko waliowachagua na kwamba maamuz yao ndo katiba ndo kila kitu,mda wao ukiisha wakitoka madarakani mambo yanabadilika kulinganà na apendavyo mtawala anaefuata,bado tuna safari ndefu sana ,
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,385
2,000
Asimsahau na yule aliuza nyumba za serikali pamoja na kununua kivuko kibovu Ikibidi amnyonge kbsa.
Teh teh teh
...dikiteta uchwara ndiyo nani? Nasikia watu wanamsema......

Subiri atakayekuja baada yake atasema kuhusu Kivuko Kibovu na Nyumba za Serikali! Kwa sasa waache wale muda wao wa kula huu.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,004
2,000
Bila demokrasia makini huwezi kujenga mfumo madhubuti. JPM anaweza akawa anataka kushughulikia ufisadi, ulege lege kazini n.k lakini bila demokrasia inayoleta checks na balances ataondoka na kila kitu chake akija mwingine tutaanza tena. Tuna watawala wenye nguvu sana kikatiba ambayo huwapa uhuru wa kufanya wapendacho hata kuwa madikiteta (hili kalisema si mwingine bali Julius Nyerere mwenyewe), tuna uchama dola (nguvu ya CCM inatokana na hili zaidi - Zanzibar ni mfano, na Tanganyika tunalijua na kuli-ishi), kulindana (mwenyewe anasema hata fukua makaburi, hata na yeye akimaliza kusiwe na wa kumhusisha na chochote alichotenda kabla na baada ya kuwa raisi). Mpaka tutakapo pata dawa ya haya mafanikio yote atakayopata yataondoka na yeye. Na haya matatu ni mambo ya kikatiba na kuiishi hiyo katiba-yeye anasema haikuwa kwenye ilani yake hivyo kwa sasa si kipaumbele chake. Kama kweli anataka legacy yake-ajenge mfumo imara-lazima ashughulikie hayo.
 
Word
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom