Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,148
- 10,571
Kwa muda mrefu, niliamini kwamba uongozi ulikuwa ni suala la kuvaa vizuri, kuwa muongeaji sana na ujasiri wa kusimama mbele za watu.
Pindi tulipokuwa shule haswa shule ya msingi basi kiongozi mzuri alikuwa mtu anayejua yote (wale much know) na kuwaambia watu wengine nini cha kufanya na mara kadhaa nafasi hizi waliteuliwa watoto wa waalimu wakuu na watoto wa walimu.
Mwanafunzi ambaye alikuwa na ushawishi na haiba na angeweza kuwashawishi wasikilizaji kufanya mambo kwa njia fulani walimu walimuogopa na kumchukia sana mara kadhaa walijikuta wakipewa adhabu zisizo na msingi ili tu kuwafanya wakae kimya.
Kuwa sahihi kila wakati, kutetea haki za wengine na kuwa na uwezo wa kuleta haki hiyo kwa wengine ilionekana ni ishara ya hatari kwa uongozi wa shule. Viongozi wengi ambao walikuwa viranja walikuwa wakizungumza kwa ukali na ubabe ili kuonesha kuwa wewe upo chini yake. Mtu ambaye angeweza kuzungumza kwa ufasaha juu ya mawazo makubwa na kuhamasisha chumba kizima.
Mtu kama huyu enzi zile alikuwa na uwezo wa kuongoza shule nzima kukataa kula chakula cha jioni, nimepata kusoma shule ambayo uongozi wa wanafunzi ukisema jambo basi kuanzia kidato cha kwanza mpaka sita tunakuwa kitu kimoja, kwa shida au raha. Picha linaanza kwenye vikao cha bodi ya shule, Kaka Mkuu pamoja na GS walikuwa wakihudhuria kama wawakilishi wa upande wa wanafunzi.
Lakini nilipoanza kukutana na zaidi na viongozi na kuangalia mienendo ya uongozi wao katika mazingira ya jamii, niligundua kuwa uongozi sio jambo la kumka tu asubuhi kunawa uso na kupaka mafuta na kutaka kuongoza watu, nilifahamu tofauti kati ya kiongozi na mtawala, nilifahamu tofauti ya kuwa msikilizaji zaidi kuliko kuwa mzungumzaji, na pia ilifahamu tofauti ya kujitoa na kutimiza wajibu.
Watu wanaonizunguka mara nyingi huwa na tabia na mwelekeo wa kuwasifu viongozi ili wapate kulinda vyeo, mamlaka, na kuendelea kupata mafanikio kupitia sifa ambazo wanaziimba kwa viongozi fulani. Lakini watu wachache huchukua muda wa kutosha kuona kile ambacho viongozi hufanya sio kwa ajili yao bali kwa ajili ya jamii.
Na kundi hili ndio kundi ambalo linaongoza kwa kuchukiwa kupita maelezo, ni kundi ambalo wakiona kiongozi yupo na tongotongo kwenye macho basi utasikia kwa uwazi kiongozi ondoa tongotongo sio wae ambao wataanza kumsifia na kudai kuwa kiongozi ana macho mazuri na anawapenda sana wananchi kiasi kwamba anakesha usiku kufanya kazi mpaka anasahau kuosha uso (Unafiki huo tena mkubwa sana).
Je kwanini unataka kuwa kiongozi ndani ya jamii yako? Jamii yako itafaidika kwa namna gani katika kujitoa kwako? Kwa mtu ambaye ana moyo wa kutaka mafanikio binafsi haya maswali atajibu kwa kutazama upande wake pekee, ila kwa mtu ambaye anatazama nafasi ya jamii yake katika utendaji wake wa kazi basi atatumia muda mwingi kujibu na hekima kubwa.
Je unahitaji kukaa mbali kiasi gani wakati wananchi wanazungumza na wewe matatizo yao, ilihali wakati wa kuomba kura, wewe mbunge na diwani ulipiga magoti na kutambaa kwenye vumbi kama kifutu aliyekosa chakula kwa siku mbili? Haina maana kutokupokea simu za wananchi wako kwa kigezo cha kubanana na vikao vya utendaji Dodoma, hao ndo waliokuweka hapo ofisini ambapo unapulizwa na AC huku wananchi wanaungua jua mtaani wakijitafutia riziki ili wapate kulipa kodi na tozo ambazo zinakulipa wewe.
Uongozi ni mchakato ambao unapaswa kushirikisha watu sio ujifungie tu chumbani pekee yako na kuja na maamuzi kwa ajili ya jamii ya watu zaidi ya elfu moja. Unapofikiriaje juu ya makundi ya jamii unayoingoza, unafikiria juu ya wengine wanaotuongoza? na sio wenyewe binafsi na familia yako.
Ninaamini kuwa tunaweza kuondoa dhana potofu kwamba kila mtu anapaswa kuongoza, wapo watu ndani ya serikali wanapaswa kuziongoza familia zao pekee, na sio kundi kubwa la watu ndani ya jamii. Kiongozi huwezi kukaa kitako kunywa kahawa na raia wako pasipo kuwa na walinzi?
Kiongozi ambaye hutaki wananchi wako wayaishi maisha unayoishi na pia hupendi kuishi maisha ya wananchi ambao unawaongoza! Kiongozi wa ajabu kweli.
Kiongozi ambaye unataka kila mtu akusifu kwa kazi yako sio suala zuri, wapo watu watakuwa na fikra tofauti na fikra zako, na lazma ukubali kutokukubaliana, wewe ni mwanadamu na makosa ni sehemu yako.
Kumbuka wewe ni binadamu, na haupo sahihi kwa 100% na hautokuja kuwa mkamilifu hivyo tegemea kukutana na watu watakaokuona tofauti, na moyo wa kiongozi mzuri ni kuwasikiliza na kuwajibu wa hoja na utendaji wa kazi mathubuti, wala sio wa vitisho na mikwara.
Kuna wakati ukikaa vizuri basi hata mapambio unayoyasikia utakuta ni unafiki pekee, yaani kila jambo unalofanya unaonekana upo vizuri basi kuna shida sehemu. Ipo siku hata ukikohoa tu watu watapiga makofi, ukijamba watu watapiga makofi ili kuonesha ni kwa jinsi gani wanakutizama kama mungu mtu.
Kwa wale wapenzi wa filamu za Uchina za miaka ya 90, filamu inaanza tu dakika ya tatu watu wameanza kupigana kisha mmoja anashinda na kumtoa uhai mwenzake, kisa tu, eti miaka 100 iliyopita Babu zao walikuwa na ugomvi mkubwa sana kuhusu pombe hivyo amelipiza kisasi.

Uongozi ni karma, miluzi mingi inampoteza mbwa.