Tunahitaji kuwa na sheria ya maadili na umoja wa kitaifa

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
mwalimu nyerere alisema uhuru bila mipaka ni wendawazimu! sasa leo hii tumekuwa na uhuru wa kupitiliza mipaka kiasi cha mtu kusimama kwenye jamii kuhubiri au kuhutubia mambo ya kurudisha jamii nyuma.

wanasiasa wanashawishi wananchi kushabikia uovu wanaofanyiwa na viongozi wao, wanasiasa wanashawishi wananchi kukataa mambo ya maendeleo kama mtaji wao wa kisiasa. hivi uhuru huu kwenye siasa hauna mipaka?

lipo tatizo pale unapomchukua mtu mmoja ukampa madaraka na ukamwambia adhibiti maadili ya taifa katika siasa na yeye anaweza kutumia mwanya huu kutumia vibaya madaraka haya kwa manufaa yake.

bado niko pale pale kwenye uhitaji wa sheria ya maadili ya kitaifa na vyombo huru vya kusimamia sheria hizi (au kuweka cheksi na balansi katika mihimili ) ili kuhakikisha siasa zozote zinazofanywa katika nchi yetu ni za kujenga taifa. yeyote anayekuja na siasa za kubomoa taifa kama short cut yake ya kupata madaraka sheria imshughulikie kabla hajaotesha mizizi na kubomoa taifa.

ukienda kwenye imani, wapo watu wanahubiri mambo ya kujenga chuki kwa wananchi wazi wazi lakini sote tunayasikia na kunyamaza. hawa ni nani anawaratibu kuhakikisha yoyote anayesikia mtu anaeneza chuki mtaani kupitia dini ana pa kupeleka taarifa.

polisi wapo lakini kutokuwepo na sheria ya kuongoza mahubiri inafanya kudhibiti mambo haya kuwa kugumu.

ndugu zangu amani hailindwi kwa kutumia silaha za moto maana silaha hizo ndizo huvunja amani bali kwa kung'oa magugu yote yanayootesha mifarakano kwenye jamii mapema yakiwa madogo kama maua au mbogamboga lakini tukisubiri yakue na kulingana mibuyu hata silaha za kisasa kabisa hatutaweza kungoa mibuyu hiyo.

tujifunze kutoka kwa wenzetu walioanguka na sisi tutafute kutembea na fimbo ili tusiangauke na sio kuandaa huduma ya kwanza tukianguka.
 
Back
Top Bottom