Tunahitaji aina mpya ya KONDOMS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji aina mpya ya KONDOMS

Discussion in 'JF Doctor' started by chigwiye, Nov 25, 2010.

 1. c

  chigwiye JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuchukue tu mfano wa mafuriko ya mto mississipi mwaka ule 2004,jimbo la new orlince liliharibika mno.Mto wenyewe haukuharibika mpaka lea mississipi ipo.Madhara yalitokea pembeni ya mto,kule wanakoishi watu.Iweje mnachukua tahadhari katikati ya mto ilhali madhara hutokea pembezoni mwa mto? Si tufikirie kukinga hata mwambao ambako ndiko huadhirika,na ndiko waishipo watu na mali zao?
  Nasema hivi haka ka-kondom kanakofunika katikati tu,kweli kanakukingeni na maambukizi ya kale kagonjwa? Mbona naona hatari kubwa iko pembeni huko,ambako mafuriko huelekea!!.Huko pembeni huko ndiko haswa kuna michubuko isababishwayo na fungus,msuguano wa mapaja (hasa kwa mabonge),kunyoa na nyembe na vipele vinavyojitokeza baada ya kunyoa.Huku tunapakingaje? Nani asiyejua hutokea mafuriko wakati wa uvunjaji wa ile amri? Haya mafuriko hutapakaa hadi mapajani ktk maungio,ambako wanaume wengi huwa wamechanika.Tuseme tuko salama kweli ktk kile kijivazi?
  Mimi binafsi naona sitatumia kondoms kwa maana ya kujikinga na VVU,hadi hapo wataalam mtakapotuletea kondoms ambazo zitafunika maeneo yote hatari,yaani iwe kama NEPRON inayotumika kukingia watoto kujichafua wakati wa kula,yeees! i mean iwe kama chupi hiviiii!! au boxer.
  Nawasilisha Hoja.
   
 2. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  So true.
   
 3. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mpaka sasa hamna utafiti wowote unaonesha maambukizi kwa njia ulio eleza, labda fanya utafiti na uje na data kabla hujaja na madai ya kondom mpya.
  Nawasilisha
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kweli hakuna utafiti wowote uliofanyika kuhusiana na madai ya mtoa mada. kwa sasa hizihizi zilizopo zinatutoa sana tu.
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  MMhhh MI Wasiwasi wangu ni kwamba, zile KONDA-MNO zililenga kupunguza mimba zisizotarajiwa, na sio kwa ajili ya mafuriko!! bytheway, huwezi kuzuia mafuriko kwa koti...hebu mwenye wimbo wa Kwetu mgeni ameingia au ule wa kijitonyama USIKU WA GIZA NENE, AU ule wa STAREHE.... AU tafuteni makala za NKOSI!!!!
   
 6. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  1. Njia sahihi ni kuacha kufanya tu.
  2.Ni sahihi kuwa maambukizi mengine hupitia njia hiyo unayoisema hasa kwa wale wenye kupenda kunyoa muda mchache kabla ya shughuli.

  Ndio maana matangazo ya kondomu husisistiza matumizi sahihi - ni pamoja na uvaaji na uvuaji.
   
 7. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 434
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hii ni dhana hatari na potofu kuliko zote nilizowahi kuzisoma. Ninavyoelewa ni kwamba kondom zina uwezo mkubwa tu wa kupunguza na hata kuzuia maambukizi ya VVU kama ifuatavyo:-
  i. Inatoa kinga kwa michubuko midogomidogo katika ngozi (microlesions) ambayo hutokea wakati watendo la ndoa kwa pande zote mbili kutokana na msuguano. Ni kupitia michubuko aina hii VVU hupenya mwilini na kuwaambukiza wahusika.
  ii. Kwa kawaida kondom zote huwekwa vilainishi (Lubricants) vyenye kemikali maalum zinazoweza kuua mbegu za uzazi za kiume (Sperm) na kwa njia hiyo kupunguza sana uwezeekano wa kubebesha mimba inapotokea ajali ya kondom kupasuka.
  iii. Vilainishi (Lubricants) hivi husababisha utelezi unaopunguza uwezekano wa kutokea michubuko na hivi kupunguza uwezekano wa maambukizi inapotokea ajali ya aina yoyote itakayosababisha uvujaji wa shahawa.
  Kwa hiyo ni heri kutumia kondom hata kama zitaleta "mafuriko" kuliko kuacha kabisa kama ulivyopendekeza kwai hatari ya kuambukizwa zitakuwa kubwa zaii ya unavyodhani. Mpo hapo wana JF wenzangu?
  N.B. Mimi ni Mfanyakazi mzoefu wa kitengo hicho kwa miaka mingi sasa.
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  aina condom mpya zinatozatkiwa ni za ulimi. tena zenye ladha mbali mbali?
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Nov 29, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  :whoo:
   
Loading...