Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,314
Ni jambo lililo wazi na bayana kuwa SIASA ndio maisha. Siasa ni maji, umeme, elimu n.k. Kwa hiari au bila kuhiari tunaguswa moja kwa moja na maamuzi ya wanasiasa ima moja kwa moja au "indirect".
Kwa kawaida siasa hufanyika kila wakati ila sehemu za kufanyia hubadilika. Wakati wa kampeni siasa za majukwaani hutamalaki kama sio "kubamba". Wakati wa Bunge siasa huhamia bungeni huku vyama vikipimana ubavu kwa hoja zenye mantiki. Bunge linapoisha kwa kutumia mwamvuli wa vyama wabunge wa chama tawala hurudi kwa wananchi kufafanua ni kwa kiasi gani serikali imejipanga kuleta "pepo" kwa wananchi. Wale wa upinzani hujenga hoja ni kwa jinsi gani serikali ilivyoshindwa kuleta "pepo" kwa wananchi.
Katika nchi yetu kwa siku za karibuni tumeona mbinu za wazi na zile za kificho zikitumika kuzuia wananchi kufanya siasa. Si bungeni wala majukwaani. Hata vyombo vya habari ambavyo navyo ni jukwaa muhimu haviruhusiwa kuchochea hoja muhimu za kisiasa.
Jambo la kujiuliza siasa zikafanyikie wapi? Au tufunge "ofisi ya msajili" wa vyama vya siasa?
Inasikitisha sana.