mtaka haki umenena, lakini viongozi unaowashauri ndo akina chiligati,sophia, makamba na wegine wa aina hiyo unategemea watakuelewa kweli, kwao maslahi ya watanzania hayana nafasi. kwanza maslahi ya chama, maslahi ya mafisadi, maslahi yao binafsi na ikikaribia uchaguzi kuwayeyusha watanzania kwa ahadi hewa, tazama leo tunajadili mabadiliko ya katiba isiyokidhi haja wao wako bize eti wawafukuze wabunge wa chadema wamesahau wananchi ndio tumewaweka hapo.sisi ndo waajiri wa wabunge wote wa ccm na cdm na wegine wasijipe madaraka yasiyo yao, hata wanaowapatia hizo nafasi wanawapa kwa kuzingatia kuwa uwezo wao ni duni hivyo kila watakaloambiwa fanya watatekeleza bila kufikiri, wapi nchi yetu inakwenda. poleni watanzania