Tuna mengi ya kujifunza kutoka Rwanda

MKEHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
716
Reaction score
1,144
Habari zenu wana bodi.

Kwanza kabisa niwakumbushe waliosahau kuwa Tanzania ni nchi ya 6 katika Afrika kuwa na idadi kubwa ya watu ikitanguliwa na Nigeria, Ethiopia, Misri, DR Congo na Afrika ya Kusini.
Hivyo Tanzania ni miongoni mwa nchi kubwa sana Afrika kwa mipaka yake, idadi ya watu na ushawishi pia. Cha kushangaza , pamoja na yote hayo nchi yetu ilikuwa nyuma sana katika mambo mengi hasa ustawi wa jamii.

Rwanda pamoja na kuwa na idadi ndogo ya watu na udogo wa mipaka yake imefanya mengi mazuri sana.
Nitayaeleza baadhi ya mambo niliyoyaona Rwanda kwa muda niliokuwa kule wa takribani miezi miwili.

Rwanda wamepiga hatua kutudizi katika suala la usafi wa mazingira na mpangilio wa miji yao tofauti na sisi. Kwa mfano jiji la Kigali ni safi sana na mpangilio wao wa ujenzi uko vizuri. Sijui kama kuna ujenzi holela uliopitiliza kama huku kwetu.

Lakini pia miundombinu yao hasa barabara zote za mijini na vijijini ziko njema. Vijiji vyao barabara zinapitika majira yote ya mwaka. Lakini pia barabara za kuunganisha mikoa yao japo ni midogo ziko connected.

Nyumba na makazi yao ni bora zaidi hasa za vijijini. Nyumba zao zimeezekwa kwa bati. Nilidadisi kujua walifanikiwaje wakasema serikali ilikuwa inawapa mabati. Ni vigumu sana kukuta nyumba ya tembe au majani.

Shule zao za umma ziko vizuri sana kuliko za kwetu. Watoto wengine mpaka wana computer mpakato. Wakati sisi hata wanaosoma form six hawana.

Lakini pia ni hodari sana kwa kilomo bora. Mashamba yao yanavutia sana. Wanaweza kulima sehemu ndogo sana lakini output inakuwa kubwa sana kwa sababu wanazingatia sana ushauri wa kitalaam. Hakuna njaa Rwanda.

Sheria inazingatiwa sana Rwanda. Hakuna kubabaisha babaisha mambo kule. Hata traffic wao hawachukui rushwa ovyo ovyo.

Wanajua lugha nyingi sana hawa jamaa. Wana uwezo wa kuzungumza kwa lugha yao kuu ya Kinyarwanda, Kifaransa, Kiswahili na sasa Kingereza. Kuna vituo vingi vya kufundisha lugha za kigeni. Usije kukaa na Mnyarwanda ukamteta ukijua hakusikii.

Wakiamua jambo hawakati tamaa. Wana umoja kwa mambo ya kitaifa. Ni marufuku sana kule kuzungimzia ukabila hadharani. Japo kuna upinzani wa kisiasa lakini hauna nguvu kabisa.

Rais wao Paul Kagame ndio kila kitu. Jamaa ni master plan. Inaonekana ana exposure kubwa sana. Mipango yake inatisha. Japo nchi ile ilikumbwa na mauaji ya kimbali lakini imepiga hatua kubwa sana kwenye nyanja mbalimbali kiasi kwamba huwezi amini yanayoendelea kule hasa kwenye sekta za ujenzi, afya, elimu na miundombinu yao.

Kama taifa tuna mengi sana ya kijifunza kutoka Rwanda.

Nimalizie kwa kuwaaga kwa Kinyarwanda

IMANA IBHAHE IMAHORO
 
Duhh wewe bila shaka ni gaidi wa tutsi maana anayempendaga dikteta Kagame ni wale wanaokula kwenye meza yake kama nyie.

Anyway mi nasubiri siku akiondoka madarakani tu au wanyarwanda wam-gaddafi kwenye culvert
 
hakuna hata moja litalotufaa kutoka rwanda
jielimishe sana then utajua kwa nini!!
 
Nilimsikia akon akisema, ametembea nchi nyingi africa lkn hakuna nchi aliyoona ipo organised km rwanda. Leo hii ukitaka kufungua biashara unapewa full details within a hour hakuna longolongo km bongo
 
Rwanda haifikii hata ukubwa wa mkoa kama Arusha. Ni rahisis sana kumanage mambo. Sasa hapa watu wa mipango toka Dar hadi waje waone kuwa kuna kijiji kando ya ziwa Tanganyika kinahitaji barabara ni lini.

Dawa ni kufanua devolution ya kweli ili mipango ifanyike karibu na wananchi na wanachi wenyewe.
 
Acheni propaganda wako njema sna, acha tuendelee na uchumi wa viwanda.
Wako njema kwa kipi? Hakuna chochote cha kulinganisha kati ya Rwanda na Tanzania Wanyarandwa ni masikini na wananjaa ya ajabu. Watutsi wanaisifu Rwanda kwasababu ni salama kwao kukaa kuliko sehemu ingine sio kwasababu ya maendeleo au kingine ila Wahutu wengi wanaikimbia na kuja kutafuta maisha Tanzania.
 
Nisikupake mafuta kwa mgongo wachapa mzee sisi hatuna cha kujifunza kutoka Rwanda kidogo ungesema watani zetu wakenya
 
Wasikutishe hao Rwanda hukuna chochote zaidi ya propaganda tu na mbwembwe
 
Sijui umejuaje sijawai kuonana mabigwa wa propaganda kama Rwanda niliwai kuishi huko
Nawajua fresh sana jinsi walivyokuwa wakiilezea Rwanda na kagame utadhani wanaishi angani sasa kwanza nlikutana na mmoja ya mfanyabishara kutoka alishangaa sana tulivyokuwa tukisema tz vyuma vimekaza na bahati nzuri nikapata fursa ya kuwatembelea mama yangu huruma niliwaonea
 
Tujifunze na kuzaa na ndugu zetu
 
Mi nilishawahi kuwa na demu wa kitutsi ila waliposafiri hawajarudi tena,nina mpango nimbandue na wakihutu nifunge mahesabu na wanyarwanda halafu nihamie DR Congo
Nalog off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…