WanaJf, nikiri kuwa mimi ni mwanachama wa CHADEMA ambapo nilikuwa kiongozi wa chama ngazi fulani siku za nyuma ila kwa sasa siyo kiongozi. Napenda kutoa mchango wangu mdogo kuhusu swala la Mh, Zitto Zubery Kabwe ambaye ni kiongozi wetu wa chama na Mbunge wa kigoma kupitia CHADEMA.
Mi binafsi natambua mchango wa Zitto ndani ya chama changu na utetezi wake katika rasilimali za taifa letu kwa maslahi ya Watanzania wote. Hakuna mpenda mabadiliko atakayebeza ukweli kuwa Zitto ni mtu muhimu sana ndani ya CHADEMA na taifa letu kwa ujumla hasa wakati huu wa mabadiliko na baada ya mabadiliko. Vilevile ni muhimu kutambua kuwa mtu muhimu katika harakati za mabadiliko anaweza kuwa mtu hatari sana wa kuhujumu mabadiliko hayo kama ataamua kufanya hivyo kwani binadamu hubadilika kila siku. Mtu muhimu leo anaweza kuwa mtu hatari sana kesho.
Zitto lazima atambue kuwa Watanzania wanataka mabadiliko hivyo hawakotayari kumvumilia mtu yeyote atakayetaka kuhujumu mabadiliko hayo awe ndani au nje ya vyama vya upinzani hasa CHADEMA. Zitto atambue kuwa unaweza kutenda mema mengi sana lakini mema yote yakafutwa na baya moja utakalotenda. Nimefanya uchunguzi mdogo mtaani kwangu nimegundua tuhuma za usaliti wa Zitto kwa CHADEMA zinafahamika kwa watu wengi sana.
Vilevile Zitto atambue kwamba watu wanaomshabikia Zitto kwenye mitandao ya jamii siyo wapendamabadiliko bali ni wapinga mabadiliko hasahasa ni maCCM na wale wanaodaiwa kuwa alikuwa akiwalipa 150,000 hadi 200,000 kwa mwezi. Hakuna mpenda mabadiliko yeyote atakayefurahia yanayosemwa kuhusu Zitto hivyo asibweteke kwa ushabiki wa maCCM akajiona anakubalika sana bali ajipime kama kweli amewasaliti wanamabadiliko. maCCM wanamdanganya ili lengo lao la kuhujumu mabadiliko litimie.
Nimalize kwa kusema kuwa wanaCHADEMA hawapendi na hawakotayari kumvumilia mtu yeyote atakaye hujumu harakati hizi za mabadiliko na vilevile hatupendi kuona na kusikia Zitto akikashifiwa na mtu yeyote ndani na nje ya chama kwani Zitto ni kiongozi wa chama hivyo lazima tumheshimu kwa nafasi yake hiyo. Pia niwaombe viongozi wetu wa Taifa watuambie ukweli ni upi kuhusu tuhuma za usaliti dhidi ya Zitto.
Viongozi wetu kukaa kimya siyo suluhu katika hili swala bali ukimya unatoa picha mbaya kuhusu uwezo wao wa kufanya maamuzi magumu pale watakapopewa mamlaka na wananchi. Watambue kuwa Watz wanataka mabadiliko hivyo wakishindwa kutuongoza kufanyamabadiliko basi wataviunga mkono vyama vingine vya upinzani bali hawako tayari kuendelea kuongozwa na CCM.
Nadhani kama ni uchunguzi basi umekamilika kwani hizi tuhuma hazijaanza leo zilishaletwa na Ben na wengine wengi sasa muda umefika wa kujua ukweli maana tunashindwa kujua nani yupo sahihi.
Nawasilisha.