kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,255
- 16,185
Ndio maana wabunge mko huko Dodoma kwenye bunge maalum la kutunga katiba mpya itakayohakikisha taifa linasonga mbele. Katika tunu za taifa msiwasahau pia Nyerere na Karume, hawa ni mafilosopher wetu.
Binafsi mimi ninamuheshimu sana Mh. Lukuvi, ni mzalendo wa kweli na anayeipenda nchi yake kwa vitendo, Lakini pia napenda kuikosoa hoja yake kwamba serikali tatu zitasababisha jeshi liipindue nchi kwa sababu ya kukosa mshahara chini ya serikali tatu. Hofu ya mh. Lukuvi sio ya kubezwa kabisa, lakini alivyoitoa sio sawa kabisa, anawatia wananchi ugonjwa wa woga (Lukuviasis) wa serikali tatu bila sababu ya msingi. Ndiyo maana Lukuvi na wabunge wenzake wa Tanganyika na Zanzibar wote wapo bungeni kuhakikisha kuwa kama itabidi ziwe serikali tatu, basi yeye na wenzake wanatunga katiba ambayo itaihakikishia Serikali ya shirikisho kupata vyanzo madhubuti vya mapato ya kuwalipa wanajeshi wasiipindue serikali kama anavyosema yeye. Atoe utaalamu wake ili hofu yake ipate majibu ndani ya serikali 3 pia, sio kuwatisha watu na kuliambia jeshi nini cha kufanya zikiwa serikali 3 zitapita.
Mh. Zitto alitoa dawa (zittoquine) ya kutibu serikali tatu. Alisema serikali zote zilizopinduliwa na majeshi yao hazikuwa za shirikisho, mfano, Misri kuna serikali moja tu lakini Rais Mossi na chama chake cha muslim brotherhood alipinduliwa na jeshi. Hii inaonyesha kuwa Kitakacholifanya jeshi lipundue nchi sio serikali moja, mbili, tatu wala mishahara tu, bali ziko sababu nyingi na mbalimbali ambazo zinaweza kutokea ndani ya serikali 1, 2 au 3. Zitto kashauri tutunge katiba itakayohakikisha kuwepo kwa utawala bora na kuwa serikali zinazokusanya kodi na kuibua vyanzo vipya vya kodi ili serikali ya shirikisho iwe na mapato makubwa ya kugharamia kazi zake. Watunga katiba wetu wanao uwezo wa kutupatia katiba ya aina hivyo kama wakiamua kufanya hivyo.
Itungwe katiba ambayo ina ubavu wa kuzilazimisha na kuzisimamia Serikali washirika juu ya namna ya kuigawia serikali ya shirikisho mapato kwa kufuata uzoefu wa nchi zilizofanikikiwa na ambazo hazikufanikiwa kuendesha serikali zao tatu, ili sisi tuizibe mianya yote ya jeshi kupindua nchi kama vile Lukuvi anavyowalazimisha wanajeshi wafanye kama zikiundwa serikali 3.
Kupitia hofu yake hiyo, Lukuvi anapaswa kuwaongoza wabunge wenzake kwenye mjadala wa namna ya kuziba mianya ya serikali ya shirikisho kupinduliwa na jeshi badala ya kuwatia hofu (Lukuviasis) wananchi wanaotaka serikali tatu.
UKAWA: kudai hati ya muungano na kusema muungano uliopo sio halali ni kututia hofu (Ukawasitis) sisi wanachi tuliozaliwa na kukulia ndani ya muungano. Kufanya hivyo ni sawa na mtoto anayewakataa wazazi wake eti kwasababu babu yake alimlazimisha mama yake kuolewa na baba yake, au kwasababu tu baba na mama yake hawakufunga ndoa kanisani au msikitini. Huu ni upuuzi mtupu, kwa watanzania walio makini hawawezi kukubaliana na hoja za kijinga kama hizi. Tunawamulika, tutahoji na mwishoni tutawakataa. lazima tukubaliane wote kwamba muungano ulikuwepo, upo na utakuwepo, kudai hati sio hoja kwetu sisi tuliokwishafaidi matunda ya muungano, kwa hili mtagombana na wengi na msiowategemea. Tuboreshe walichofanya Nyerere na Karume sio kukibomoa.