Hahaha huyu huyu Halima Mdee aliyekuwa anafukuzwa bungeni kila siku na ndugai tena kwa kashfa leo mnasema alikuwa na mchango mkubwa bungeni?!
Chama cha Chadema akiwemo huyo huyo Halima Mdee waliongoza kuuonyesha umma kwa kuonyesha kura feki za ccm zilizokuwa zimeshajazwa kuingia vituoni, hilo lilituonyesha uchaguzi haukuwa huru na haki, leo huyo huyo anapokubali haram anaonekana shujaa?!
Chadema haitambui uchaguzi uliopita kwanini ikubali viti maalum?!
ACT wakiwa CUF hawakukubali kushiriki serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kwanini leo?!
Usaliti ni dhambi kama kuua, na nidhambi kama kuiba, hakuna dhambi kubwa kushinda nyingine, kwa walilolifanya ni usaliti wa wananchi kwa maslahi binafsi siyo ya taifa wala wananchi.
Wako 19 hawana tofauti na COVID-19, wame saliti umma wameamua kujinufaisha ni nje na malengo ya chama.
Hivyo COVID-19 hawatufai wacha waende, tuta recruit wengine wanawake hawajaisha.