Tumesambaratishwa ukweni

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,968
Kwa wenye kumbukumbu mtakumbuka niliahidi kwenda ukweni kupambana na nikasema nimepata majembe, uncle wangu aliyeahidi atafanya maajabu katika bargaining power.

Kweli siku ikafika tukaenda, kufika kule tukakuta vizee kama 10, si kawaida kabisa maana zoezi hili linahusishaga watu kama 3 toka kila upande.

Mazungumzo yalipoanza majembe yangu yalizingilwa kila kona, kwa maneno rahisi tulisambaratishwa kwa hoja, nilijizuia kuongea ila kila tukienda pembeni kuteta nawapa mbinu.

Cha kushangaza wakifika uwanja wa mapambano point zote zinayeyuka, natamani kusaidia ila najizuia, mwisho wa siku wakakubali tu tulichoombwa, tulichokifanya ni kulipa kiasi na kuahidi baki tutamaliziaga siku za usoni, kuna ka msemo mahali haimalizwagi.
 
mmh mahari ndo inatolewaga hivyo kweli? au mila tofauti?
 

Mlikuta wazee au vizee? Unajua tofauti yake?
 
Kwa jinsi nilivyosoma hii thread nimeelewa kwanini mlikuwa mnasambaratishwa
 
mmh mahari ndo inatolewaga hivyo kweli? au mila tofauti?

tuliomba tu, ila utaratibu sivyo, kwenda na kurudi ingeleta usumbufu na gharama zisizo za msingi.
 
Hahahahahahah mjiomba alikua na mbwembweee kama gauni la Harusi teh teh

wee acha mkuu, njiani mbwembwe nyingi, kufika pale akatulizwa, eti leo nitafanya maajabu, wapi bwana....
 
walitukaba kwa milioni 3 mkuu.
 
Yaani wewe ndiwe uliyekuwa ukitoa mbinu za ushindi JEKI? Kusambaratishwa hakukuwa kunaepukika...
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Kbd
Hahahahahahahah JEKI maajabu yakuwa pointless haahahahaha
wee acha mkuu, njiani mbwembwe nyingi, kufika pale akatulizwa, eti leo nitafanya maajabu, wapi bwana....
 
Last edited by a moderator:
Pole.... Maneno ya kufundishwa siku zote mtihani
 
Mahari hata iwe elfu 50 hautakiwi kuimaliza.Mahari haimalizwi.Safi sana mkuu.
 
Huna adabu kabisa unaita ndugu wa huyo mkeo eti vizee..umelaanikamsana wewe na kufitinika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…