Natamani tungependana
Na sio kutamaniana
Natamani tungeendana
Na sio kugegedana
Natamani zingerandana
Hisia kushabihiana
Lakini zatofaitiana
Zako ni kufurahishana
Zangu ni kupendana
Ni kuzuri kufurahishana
Kuendane na kuahidiana
Milele kupendana
Milele iso kimalagasiana
Natamani kukumbatiana
Natamani kuliwazana
Natamani kufarijiana
Natamani tungeendana
Tuongeze kuwasiliana
Tupunguze kulaumiana
Tuongeze kubusiana
Tupunguze kuhitilafiana
Yetu yawe ya mfano
Mapenzi yaso kikomo
N.B
'Milele' kwa kimalagasy (lugha izungumzwayo Madagascar) maana yake ni kugegedana