Dr hamisi amejitoa jf au anasubiri wakati wa bajeti ya wizara husika?
Ndg. bado nimo ndani ya JF na nitaendelea kuwemo!
Sikupenda sana kuja kujadili hapa. Lakini kwa kuwa nilifanya mgomo huu publically basi naomba nitoe maelezo kidogo.
Wanaosema unafiki, hawajui maana ya uwazi. Ningeweza kuamua kunyamaza na machungu yangu moyoni na nikaenda kuikosoa na kuikwamisha bajeti ndani ya Bunge, hapo ningekuwa mnafiki na msaliti mkubwa kwa kamati yangu. Ili hayo yasitokee nimefanya mgomo na nimedhihirisha wazi hasira zangu na kutokuridhika kwangu. Sasa tumekubaliana tutakaa tena kama kamati tukiwa huku Dodoma na kuweka mambo sawa.
Kilichotokea hakikuwa sahihi kwa kanuni za utendaji za kamati za Bunge - ambazo zikiwa kazini, zinafuata kanuni zote za Bunge, kwa sababu zinafanya kazi kwa niaba ya Bunge zima!
Kilichotokea ni kwamba; Wizara iliwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya mwaka unaoisha na kisha mapendekezo ya mapato na matumizi kwa mwaka huu unaokuja. Tukaanza kujadili, mimi, pamoja na mambo mengine niliibuka na matatizo mawili ambayo kwenye majibu ya wizara sikuridhika.
Haya yaliwahusu madaktari bingwa 61 waliohamishwa kwa njia ya tangazo gazetini bila kupewa barua, na sasa wengi wao wamezisusa ajira hizo, wameamua kwenda kufanya kazi kwenye private sector, ambako wanalipwa vizuri zaidi na hawanyanyaswi, na wengine wanajipanga kwenda nje ya nchi kwenye green pastures.
Wizara siku zote badala ya kuwa rafiki kwa wataalamu imekuwa ikiwasukuma waichukie na waikimbie. Wataalamu wakienda kwenye private sector, wagonjwa maskini wanatibiwa na nani? La pili lilikuwa ni la usanii unaofanywa kwenye kitengo cha figo Muhimbili, ambacho Mhe. Rais amekihangaikia sana kukianzisha, sasa pale kuna mtu anakwamisha, na mimi simjui na wala sikutaka kumtaja, nilitaka kujua kwa nini mtu huyo ana-frustrate wataalamu na wafadhili wa kutoka Norway, ambao ndiyo walitupa mashine za kuchujia damu (dialysis) na wako tayari kuleta nyingine (yeye anazikataa anadai anataka kununua nyingine kwa fedha za serikali).
Chuo hiki kinataka sasa kuvunja uhusiano na kitengo hiki na kuacha kuwafadhili wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma huko. Huduma hii si itakufa?
Pia tulijigawa kwenye vikundi kazi vya watu wachache wachache na mimi nilikuwa na wenzangu 5 tukapewa kipengele cha matumizi ya kawaida (recurrent expenditures). tulivyoanza kuchambua subvote (kifungu) ya kwanza ya administration and general, tukagundua uozo mkubwa, kwamba activities zilizokuwa kwenye MTEF haziendani na fedha zilizowekwa kwenye Randama na kwenye budget book.
Kwa maana ya Budget book ina figure za ujumla jumla, pia na randama vivyo hivyo; ili uweze kunyumbulisha na kuelewa mambo ni lazima uone zile figure za ujumla jumla zinamaanisha nini?
Na hapo unarudia kinyume nyume kule kwenye MTEF, ambamo utakuta sasa activities imeelezewa in detail. Pia tukagundua kulikuwa na copy and paste nyingi. Kikundi kazi chetu kikashindwa kuendelea na subvotes nyingine baada ya kujiridhisha kwamba bajeti haikuwa serious kama inavyopaswa.
Wizara walipokuja kusikia ushauri wetu tukawaomba warudi wakaandike MTEF nyingine ambayo iko serious kidogo na inaendana na ukweli ili sasa tuweze kuja kuendelea na kazi ya uchambuzi.
Bila shaka hata wewe unayesoma hapo umenielewa vizuri kwamba baada ya kurudi kesho yake tungetakiwa turudi kwenye vikundi kazi vyetu tuianze upya ile kazi baada ya Wizara kurekebisha MTEF, au siyo?
Sasa kilichotokea sicho! Hatukurudi kwenye vikundi kazi na badala yake Mwenyekiti akishirikiana na wajumbe wachache walianza kutetea kwamba tuelekee moja kwa moja kwenye kusoma na kupitisha kifungu kwa kifungu, na kwamba eti kama kuna mtu ana marekebisho au swali basi atauliza na atapatiwa majibu na Wizara pale pale, na hivyo tutaipitisha bajeti na marekebisho.
Wachache tuligoma na hilo zoezi likasonga mbele. Na kwa yale majibu mepesi mepesi yaliyotolewa kwa maswali yangu inakuwaje? Nikaambiwa itapangwa siku nyingine ya kusikilizwa! Sasa mimi nikashangaa imekuwaje, mbona huu si utaratibu wetu hata siku moja? Kunani?
Nikipewa muda wa kuongea, nikisimama na kuanza kujenga hoja zangu, siruhusiwi kumalizia sentensi hata moja, ilimradi tu inahusu maswali magumu! Nikaona huu si utaratibu wetu siku zote tangu nimeingia Bungeni na kwenye kamati yetu, imekuwaje leo???
Niliamua kususia kikao. Nikatoka. Maana sisikilizwi na siwezi kukaa kwenye kikao ambacho mimi haki yangu ya kusikilizwa inabanwa, sasa kwa nini mimi niwasikilize wengine?
Sielewi kulitokea nini, labda ni ugeni wa Mwenyekiti, ni upofu (sijui umesababishwa na nini), au ni nini?? Bado najiuliza.
Japokuwa wanakamati wameamua tukutane hapa Dodoma tuyaongee na kuyaweka sawa haya mambo.
Wakatabahu,
HK.