"Tumekubali kuburuzwa kupitisha bajeti ya afya"-Dr.H.Kigwangalla

serikali inavyotishia kufunga vituo vya afya binafsi vinavyotumia madaktari wa serikali imefikiria au inaropoka?sasa hivi vituo vikifungwa wagonjwa wake waende hospitali zipi?kuna utafiti wowote unaonesha takwimu za madaktari wanaotoroka vituo vyao vya kazi na kwenda kwenye viosk au wanachanganya part time job na utoro?je serikali imejiuliza tatizo gani la msingi linawafanya madaktari hawa(kama wapo) watoroke vituo vyao vya kazi?

Kweli kwa bajeti hii ilivyo ni dhahiri mliburuzwa!
 
Kila nikikumbuka siku ilivyopitishwa najeti ya wizara ya Afya kwa kweli uhuni mwingi sana ulitumika kuhakikisha bajeti inapitishwa. Majibu ya mheshimiwa Waziri yalikua ni ya kisiasa sana na sio ya kiutendaji na yenye kuonyesha mabadiliko katika sekta ya Afya. Kuna baadhi ya mawaziri walisimama kidete kusaidiana na Waziri wa Afya kuhakikisha bajeti inapita. Na ndio siku ile hadi ikafikia hatua wengine wakawaita wapinzani Wanafiki na miongozo ya spika ilikua mwingi mwishoni na tulishuhudia Naibu Spika akikataa kuitikia Baadhi ya Miongozo na kufunga Kiakao kwa kulazimisha huku wabunge wakiendelea kubishana

NOTE: Hapa napo inawezekana watu walichukua hela kuhakikisha Bajeti inapita
 
You are right!!! Ndiyo hayo Dr. Bana anasema bunge makini. Bajeti hiyo pia haikupashwa kupita. Ilikuwa hovyo bila kuaddress issues ngumu za afya ya watanzania!!! tene afya ya msingi tu. Imeacha maswali mengi kuliko majibu.
 
wakuu tuna uhakika gani kwamba kamati hii haitaburuzwa tena katika suala la mgomo wa madaktari?
 
inawezekana kabisa chanzo cha mgomo unaoendelea unatokana na bajeti mbovu iliyopitishwa kibabe na bunge letu.umkini unahitajika kwenye suala hili,tusirudie makosa.
 
Naomba kukuuliza Dokta Hamis, hivi nyie madokta mnaohama na kushika nafasi zingine nje ya professional zenu huwa mnaweka utaratibu wa kutoa tiba at least kwa kujitolea katika kipindi chenu cha mishe mishe? Na hii ningependa kujua kwa wanasiasa wenye fani zingine kama Mainjinia, Maprofesa n.k....nimeuliza maana naona kuna utititiri wa madaktari sijui kama wote ni wa tiba au elimu lakini wengi hapo mjengoni na hata kwenye maofisi mengine sielewi kama ndo wameshaachana na fani au huwa wanapiga "deiwaka" wanapohitajika.
 
Maumivu ya kichwa yalianza polepole.....sijui naelekea kwenye psychosis.

Muhimbili.... KCMC....Morogoro....Dodoma...BMC....Amana, Mwananyamala,Temeke...Mbeya RH...

Mama yangu wee!! Muhimbili imefungwa...kituo cha utalii kwa asiye mtumishi wa hapo.

Afana lek!!
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii anaitwaje? Naomba anayefahamu wajumbe wa Kamati hii atutajie majina yao,tupache picha ya watu aliokua anazungumzia Dr. Kigwa.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii anaitwaje? Naomba anayefahamu wajumbe wa Kamati hii atutajie majina yao,tupache picha ya watu aliokua anazungumzia Dr. Kigwa.
mama sitta,ndugulile na maji marefu ni baadhi yao.
 
Back
Top Bottom