Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,475
- 29,687
Sisi ni watanzania katika nchi huru
Tumechoka kuonewa na polisi
Tumechoka kubambikiwa kesi za uongo
Tumechoka kupigwa ili kutuliza frustration za ugumu wa maisha ya askari
Tumechoka kutozwa rushwa kwa kila jambo linalohitaji huduma ya polisi
Tumechoka kusikia uongo wa polisi kila wanapokiuka haki zetu
Tumechoka kuwa chanzo cha kitoweo cha askari wa usalama barabarani
Tumechoka kuzika ndugu zetu na rafiki zetu wanaofia mikononi mwa polisi
Tumechoka kuuguza majeraha yanayotokana na polisi
Tumechoka kukataliwa haki yetu ya dhamana kwa ubinafsi wa polisi badala ya sheria
Tumechoka polisi kutumiwa na matajiri wachache kutunyima haki zetu
Tumechoka kuona polisi wakigeuzwa kuwa chombo cha ukatili cha wanasiasa
Tumechoka kuona polisi wakijifanya miungu wadogo katika kushughulika na raia
Tumechoka kuchukuliwa na polisi kama watu tusio na uwezo wa kufikiri
Tumechoka kuona haki zetu za kiraia zikiwekwa mikononi mwa polisi pasipo utashi wetu
Si unyonge wetu uliotufanya tukubali kuonewe na polisi muda wote huu, tuna nguvu ya wingi wetu
Si ujinga wetu unaotufanya tudhalilishwe na polisi katika nchi yetu wenyewe, tuna uvumilivu
Si umasikini wetu unaotufanya tuwavumilie polisi muda wote huu, tuna amani
Lakini sasa tunasema basi inatosha
As long as jeshi la polisi wanaajili failures katika mitihani-div 4 and 0, then utendaji wapolisi hautabadilika. Ukiacha akina Kaqmuhanda ambao wanatafuta kuifurahisha CCM, with education naamini tunaweza kulibadilisha jeshi letu. lazima katiba itamke wazi kuhusu polisi na ukatili wao.
Ina maana kua na mapolisi failures ndio sababu ya kuwa chombo chenye mamlaka ya kuonea mpaka kuua raia??sio kwamba muundo na uongozi wao kua mbaya na kufuata matakwa ya wakubwa wao??? sio kuwa na serikali yenye kutumia vyombo vya usalama kwa maslai yao binafsi??sio sheria mbovu zinazowakinga wao kama vyombo husika vya ulinzi??
Hatuna jeshi la polisi! IGP ni shemeji wa dhaifu! jeshi halina nidhamu! wanababimbikia watu kesi,Jeshi linanuka rushwa! kuingia kituo cha polisi bure kutoka na hela.Jeshi la polisi ni tawi la magamba!
Haya, jana tu nimeweka hii thread, leo tunasikia Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Albert Buchafwe amenusurika kuuawa kwa risasi na Mkuu Msaidizi wa Kituo cha Polisi Nyakato, Abubakar Zebo. Halafu kwa ujinga usio kifani kama vile watanzania wote ni mambumbumbu wa kudanganywa kirahisi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow, bila hata kumhoji alieyetaka kuwawa, anasema ana uhakika ni bahati mbaya kwani jeshi lake lilipata taarifa za Kiintelijensia za kuwapo kwa majambazi wakidaiwa kutumia gari sawa na la ofisa huyo. (Na kwa jinsi magari yanavyofanana Tanzania kama polisi wanashambulia gari kwa kuwa tu linafanana na wanalotafuta basi wao ni polisi mbumbumbu kuliko wote duniani)Kuna askari waliombambikizia mama mjane kesi. Wakamptupa rumande bila kujali ukiwa alionao wa kufiwa na mumewe gafla aliyemwachia watoto saba akiwapo wa mwaka mmja na miezi. Mama huyo analilia rumande. Watoto wake wanasota bila baba wala mama. Mhusika wa kesi alitoa rushwa ya kutosha kwa polisi wakamwachia na kumchua huyu mjane maskini asiye na mtetezi na kumfungia badala ya yule mhusika.
Je hawa polisi waliofanya hiki kitendo watasalimika? Kilio cha huyu mjane ambaye amesotea rumande sasa ni mwezi wa tatu kitaliacha hili taifa katika usalama? Kwa uhakika hana cha kufanya isipokuwa kulia na kusali. Ipo siku moja kilio chake kitayafikia masikio ya mwuumba wake. Huyo Mwuumba aafanya nini kwa hawa waliomtendea unyama kama huu masikini huyu? Tusumbiri tuone kwani maandiko yanasema nitakisikia kilio cha majane na yatima. Polisi jiangalieni sana hii rushwa imewapeleka mbali mno!