Tume ya Rais

mizambwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2008
Posts
4,421
Reaction score
1,792
Watanzania tumeshuhudia TUME nyimgi zikiundwa na Marais. Nakumbuka Raisi Mwinyi aliunda Tume ya Maoni ya Wananchi kuhusu Vyama Vingi. Na matokeo yake tulielezwa na yakafanyiwa kazi.

Rais Mkapa aliunda Tume nyingi mfano tume ya Rushwa iliyoongozwa na jaji Warioba; na nyingi siwezi hata kuzitaja. Matokeo yake aliyajua mwenyewe kwani hayakuwekwa hadharani

Rais Kikwete ameunda na anaendelea kuunda Tume nyingi na matokeo yake hatuelezwi na pia hayafanyiwi kazi. Mfano tume ya hivi karibuni kuhusu Mgomo wa Madaktari. Na taarifa alikabidhiwa Spika wa Bunge. Tulitaraji tutaelezwa Bunge lililoishia jana. lakini nayo kimya.

Tume ya kufuatilia mauaji ya Songea, hadi leo kimya. Afande Chagonja na timu yake wamesharudi.


Je, wadau kuna umuhimu gani wa kuunda hizi tume? Je, pesa zinazotumika zimepitishwa na Bunge lipi?



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Na hata hii tume ya katiba mpya, usitarajie kitu kipya. Mkubwa Akija kukuta kipengele kinachosema "Rais na mawaziri waliobainika kuiba pindi walipokuwa madarakani lazima washtakiwe". Katiba itatupwa hiyo....
 

Ni kitu kigumu sana kutangaza maoni ya tume iwapo hata wewe kama rais unaguswa. Kwa mfano mauaji ya Songea hata Rais anahusika.
 
Na hata hii tume ya katiba mpya, usitarajie kitu kipya. Mkubwa Akija kukuta kipengele kinachosema "[B]Rais na mawaziri waliobainika kuiba pindi walipokuwa madarakani lazima washtakiwe[/B]". Katiba itatupwa hiyo....

Kweli lazima ataifunika tu. Akikuta yanayomkaba hatokubali. Vinginevyo atajifanya kama hakuliona na lisiwekwe katika katiba


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Tume ni tactic mkuu,

Joto linakuwa kubwa na usipounda tume hakitaeleweka. sio tanganyika tu sehemu nyingi hii kitu inatumiwa sana kupunguza munkari.

Nabii gani mtarajiwa usiojua mambo madogo kama haya
 
Tume ni tactic mkuu,

Joto linakuwa kubwa na usipounda tume hakitaeleweka. sio tanganyika tu sehemu nyingi hii kitu inatumiwa sana kupunguza munkari.

Nabii gani mtarajiwa usiojua mambo madogo kama haya

NDUGU UNATAKA KUNIVUNJA MBAVU KWA KICHEKO, hunihurumii hizi MBAVU nilivyokonda na kuwa mifupa mitupu!!!

Utabiri wangu unaonyesha kuwa Tulipo ni Pabaya na Tunakoelekea ni Pabaya zaidi.

Hivyo tuchunguze umuhimu wa hizi tume zisizo kuwa na majibu.


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…