Tumbua majipu

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,492
4,770
TUMBUA MAJIPU.

1)Ukweli yanaumiza,maumivu ni makali.
Ni lazima kumaliza,tena kuyatupa mbali.
Na dawa yake fukiza,hata kama njia ghali.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope.

2)Wengi wanayachukia,wala hakuna mithali.
Heshima itarejea,yakionja siri kali.
Ile waloitendea,sasa waonja miali.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope.

3)Hata kule bandarini,nako wachome sindano.
Ganzi ifike moyoni,wakome hu mpambano.
Wawe makini kazini,na waache maagano.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope

4)Hata wale wa nishati,nako hakuna lumbano.
Nao wapige manati,kiwakolee kibano.
Hata pesa za kamati,wasile kwa mkutano.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope.

5)Papa nayo manyangumi,hayo kwetu ni kidonda.
Yafaa kupigwa ngumi,hata kama yatakonda.
Kwanza yakate ulimi,yasitoroke na honda.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope.

6)Ukate yao makucha,yanyooke yalopinda
Hata yaliyojificha,tuyatoe kwa vibanda.
Keki waliyoificha,watoe isije vunda.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope.

7)Karibu yatafumuka,na majipu yatatoka.
Punde yanaja umbuka,karibia yaibika.
Aibu tena ya myaka,isoweza elezeka.
Jembe tumbua majipu,kidonda hiko kipone.

Shairi:TUMBUA MAJIPU.
mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382386
0655519736
iddyallyninga@gmail.com
 
TUMBUA MAJIPU.

1)Ukweli yanaumiza,maumivu ni makali.
Ni lazima kumaliza,tena kuyatupa mbali.
Na dawa yake fukiza,hata kama njia ghali.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope.

2)Wengi wanayachukia,wala hakuna mithali.
Heshima itarejea,yakionja siri kali.
Ile waloitendea,sasa waonja miali.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope.

3)Hata kule bandarini,nako wachome sindano.
Ganzi ifike moyoni,wakome hu mpambano.
Wawe makini kazini,na waache maagano.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope

4)Hata wale wa nishati,nako hakuna lumbano.
Nao wapige manati,kiwakolee kibano.
Hata pesa za kamati,wasile kwa mkutano.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope.

5)Papa nayo manyangumi,hayo kwetu ni kidonda.
Yafaa kupigwa ngumi,hata kama yatakonda.
Kwanza yakate ulimi,yasitoroke na honda.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope.

6)Ukate yao makucha,yanyooke yalopinda
Hata yaliyojificha,tuyatoe kwa vibanda.
Keki waliyoificha,watoe isije vunda.
Jembe tumbua majipu,tumbua usiogope.

7)Karibu yatafumuka,na majipu yatatoka.
Punde yanaja umbuka,karibia yaibika.
Aibu tena ya myaka,isoweza elezeka.
Jembe tumbua majipu,kidonda hiko kipone.

Shairi:TUMBUA MAJIPU.
mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382386
0655519736
iddyallyninga@gmail.com

Safi sana kiongozi, nimefurahi mtumbuaji jasiri kapatikana, wenye majipu hawana pa kutorokea hawawezi tena walizoea kuweka vimulimuli kwa wapambe na mtaani kwao, wenye majipu wamebaniwa passpoti, bado watang'ang'aniwa kama mpira wa kona. Kwani shilingi na dola bado wanazo nyingi.Watazirudisha kwa kwa kudhaminiwa kupitia wapambe wao, wao wakubali yaishe
 
Back
Top Bottom