Tuliowahi kuvuta bangi tukutane hapa

Gaddaf i06

JF-Expert Member
Nov 14, 2022
1,759
2,795
Sheria imewekwa ili ivunjwe.

Tangu nilipoanza kusikia habali za bangi, sikutaka kuamini hivi hivi bila kuifanyia test!

Bangi niliipata kiulaini tu (kijijini), nikaiandaa vema kabisa na tayari kwa matumizi!!
Bwana wee! Nikapanga ratiba zangu vizuri ili baada ya kumaliza kazi zote niende sehemu TULIVU nivute sasa! (nilijuwa naweza kutokewa na lolote ndiyo maana nikajipanga)

Jioni nikaenda zangu mlimani nikiwa na msokoto wangu mfukoni pamoja na kiberiti.. Nilivuta ile kitu mpaka ikaisha kabisaa, nami nikatulia kusubiri matokeo!!

Nilikaa pale kama dak 10 bila kuhisi chochote wala hakuna kilichotokea.

Nikahisi labda nimeitengeneza vibaya, nikaenda kufanya udadisi huko mtaani japo sikusema lengo..

Nilipewa somo na nikalifanyia kazi sikuona utofauti wowote na mwanzo!

Mwaka 2016, nikakutana na bosi flani mwanachama mzuri tu nikamwambia namimi natumia hiyo kitu(ktk stori za hapa na pale) jamaa hakuwa mchoyo!!

Aah nikakata tamaa nikasema bangi ni UTAPELI bora unywe konyagi
 
Mkuu selewi jinsia yako?

Katika mada ulivuta majani ya mwarobaini pata yenyewe hii ardhi niliona inamatuta mamaee tena first pafu
kilichokudhuru ni moshi wala si kwasababu ulikuwa moshi wa bangi. Chukua paper ya daftari ichome uvute ule moshi uone kama hutoona mbingu znashuka! Bangi inaogopeka kwenye mindset za watu kiuhalisia bangi haina tatizo na mtu
 
Aise mzee hiyo kitu acha kabisa
Mimi nakumbuka niliitest enzi hizo Niko form 4, Kuna ndugu yangu alikuwa anatumia nikaona isiwe kesi Wacha na Mimi nitafute arosto!

Aisee baada ya pafu kadhaa, break ya kwanza nilijikuta chooni!! Ewalaa nikaanza kutafakari kilichonipeleka chooni nkajikuta hata sielewi nimefikaje na nimefata Nini.

Picha la pili likaanza muda wa chai, nikashangaa chupa ya chai Iko mdomoni, hata sikukumbuka kama Kuna kutumia kikombe !!

Kiukweli ilikuwa ni siku ya vituko, nashukuru tu tulikuwa peke yetu nyumbani na Chali yangu .

Ila nilipata funzo.
Aisee bangi sio powa. Tokea siku ile Niliapa sitorudia kujaribu kuvuta moshi wa huo mmea uliotaka kunitia uchizi!!.

Nawasilisha!!
 
achana na bangi kwanza: ulishawahi kuvuta sigara?
 
Back
Top Bottom