jiwekuu770
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 2,246
- 1,646
Wako kibitiMwaka 2013 Dar
Nilitapeliwa elf70 na watu wanaojifanya wanamadini kumbe mawe!!....bado had Leo nawatafuta
Ha ha ha ha2010 mitaa ya msimbazi k/koo nilinunua kipande cha sabuni kwa 17,000 .Halafu baada kama ya wiki kupita yule jamaa nilikutana naye maeneo ya mchikichini k/koo ,nikampa salamu naye alinikumbuka,akanichangamkia kwa bashasha,then nikaachana naye bila kumuuliza chochote .maana kwa Hali niliyomkuta nayo sizani hata jero alikuwa nayo.teh teh teh
Buku samehe tu mkuuNakumbuka mwaka 2007 Nilitapeliwa ubungo. Jamaa alikuwa anauza vocha aliingia kwenye gari nkampa elfu mbili anipe ya buku. Akanipa akanambia subiri chenji. Akawa anaendelea kuuza kwa abiria wengine. Alipomaliza akashuka kwenye basi akakimbia. Yani buku yangu ilienda hivi hivi. Mungu amzabe.
Ndo tufahamishe maana hawa watu kila cku wanaUpdate mbinuNashukuru mungu mpaka sasa sijatapeliwa kwasababu njia zote za kutapeliwa nazifaham
Watu huwa wanasahau kuna keshoNiliwakutapeliwa huku nikijua natapeliwa ili nione mwisho wake tena na Rafiki yangu sh 150,000 kuwa Kuna bosi anamfahamu ili aniunganishe na jambo Fulani x huku nikijua hamfahamu na wala sikuwahi kumwambia kuwa humjui.
Mungu alimpa adhabu mbaya sana baada ya Mke wake kapata mimba alinifuata ili aiote kwasababu haikuipanga.Acha mkeo azae tu akakataa na kutafuta madokta wa kuitoa lakini mimba iligoma
Na mwishoni Mke akajifungua mtoto kwenye ubongo tahira.
Huwa inaniuma sana kwasababu ni miaka 20 imepita Sasa toka kutapeliwa na mtoto tahira kuzaliwa.
Yaan we ruby wa yamoto mi sijaelewa utapel wako ulitokeajeAssist na Raimundo lakini mwisho wa siku ikageuka nimekopwa penzi.
Yaan we ruby wa yamoto mi sijaelewa utapel wako ulitokeaje
Toka nilivyokuwa mdogo mpaka leo, mama yangu ananiambia changu ni chake, na chake ni changu. Ananiitaga baba yake. Hii ilimtokea yeye, but since it was mine too, acha nitoe ushuhuda.Kama funzo kwa wengine na kujua mbinu za matapeli toa ushuhuda hapa
Naanza na mm mwenyewe
Mwaka2015😀odoma
Nilitapeliwa Simu ya itel Mpyaaa!! Kwa kubadilishana na Sony experia copy!!
Na kumuongezea lak1... Kuja kushtukia baada ya dk 5!!
Funzo:Haraka na tamaa cyo nzuri
Shuka ushuuda wako hapa!! Tukomeshe tabia hii
Daahh hii story natamani ningeijua zaidi , imetake my attention!! Mkuu ebu endelea kutiririkaToka nilivyokuwa mdogo mpaka leo, mama yangu ananiambia changu ni chake, na chake ni changu. Ananiitaga baba yake. Hii ilimtokea yeye, but since it was mine too, acha nitoe ushuhuda.
2011, mama alikutana na kaka mmoja aliejifanya anafanya kazi kampuni X ya simu. Akawambia kampuni ilimpa tenda ya matangazo, but alihitaji more money. Kweli Mara ya kwanza mama alimpa 40m akapata na faida juu ya 30m, kwa maama tulirudishiwa 70m in 3 months. Kumbe ilikuwa trailer tu.
Huyu jamaa alikuwa anaendesha marange, land cruiser latest na BMW X5. Anapiga suit tu. Sehemu za kumeet ni golden tulip au White Sands... High class places.
Akaja Mara ya pili, now akasema tenda ya TZ yote, anahitaji 400m. Mama alimuamini sana. Akakopa mkopo bank wa mil 150, akauza magari, viwanja, akampatia 400m. Hapo home maisha yalichange kabisa, mama anatuhakikishia its temporary. Hakujua kuwa its gonna be for a very long time. Jamaa alivyopewa kesho yake akapotea.
Tulikuja kumpata South Africa, tukamuweka ndani, anasema na yeye katapeliwa na kazi alikuwa hafanyi kampuni ya simu X, na magari yalikuwa ya kukodi. Jamaa alikuwa hana kitu kabisa. Katupa Nyumba yake gofu... Matengenezo karibu 50m. Gorofa letu Mara ya mwisho ilifanyiwa valuation ilikuwa 556m. Tukashindwa kurudisha Nyumba imeuzwa. Leo hii tunapokaa. Naandika hapa nalia. Acha nifungue kitabu niendelee kusoma. Nitakujengea tena mama, changu ni chako.
-callmeGhost
eidha bado umdogo sana ama hujapitia purukushani za maisha na changamoto zake,ama unaishi shamba.inatapeliwa serikali,sembuse weweNashukuru mungu mpaka sasa sijatapeliwa kwasababu njia zote za kutapeliwa nazifaham