Tuliombee Taifa tusimwombee Rais pekee

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Kitu kizuri siku zote akiwezi kuonekana wakati unacho, Mara TU utakapokipoteza ulichonacho ndipo utaona uzuri wake.

Mhe. Rais anafanya haya yanayotekea kwa sababu labda mazingira yanamfanya afanye hivyo, uzuri wa haya anayoyafanya si rahisi sisi tuliowengi kuyaona ila siku itafika pale ambapo nukuu za matamshi yake zitaanza kutumika kuiongoza jamii pakwenda.

Tuwe wavumilivu maadamu tumemkabidhi nchi huku tukiiombea Tanzania iwe salama kuruhusu ujio wa utawala mpya.Tusipoiombea Tanzania tukamwombea Rais pekee yamkini matendo yake machache yasiyomazuri yanaweza kutusababisha tukashindwa kuelewana na kufarakana, lakini tukiliombea taifa basi tutakuwa na ivumilivu wa kukemeana na mwisho tutafika atakapotufikisha na akishuka Basi tutamtafuta dereva mpya wakufukia mashimo na nyufa za JPM.

Tuelekeze maombi na Dua zetu kwa mama Tanzania, Tanzania ikiwa mikononi mwa Mungu hata viongozi wake watakuwa mikoni mwa Mungu na watatuvusha salama.
 
True...Dua kwa Taifa ni Dua kwa wananchi na kila kilichopo ndani ya Taifa husika. Tujenge tabia ya kuliombea Taifa na si kumwombea kiongozi
 
Mimi kwa dhati ya moyo wangu naliombea taifa usiku na mchana; na kwa dhati ya moyo wangu simuombei magufuli wala Rais!
 
Neno, Tuliombee taifa lipate Baraka na kujitambua. Mliokaribu nae mwambieni Muumba hadhihakiwi, anamtaja mara nyingi kinafiki na kutenda kinyume chake.
 
Back
Top Bottom