Norshad
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,207
- 12,505
Wakati tupo wadogo niliwahi kusikia kuna watu wenye uwezo wa ku funga mvua, Kama hili swala linawezekana na iwe hivyo maana wengi tunaihitaji mvua lakini ya kiasi, hii mvua ya inayoendelea sasa imepitiliza na kuwa maafa kwa baadhi ya wananchi, nasema kwa baadhi sababu wapo wanaotamani iendelee hata kwa mwaka mzima kwa maslahi yao..mwanzo tulifurahi tukasema kheri imekuja bei ya mahindi itashuka na mazao mengine yatanusurika ajabu ikapiga ya wastani hindi likasimama vizuri, ikaendelea kupiga hindi likazidi kuwa refu halibebi, na mwisho wiki hii imekuja kuyasomba na mahindi yenyewe yote, yaani kwa mvua hizi tutarajie bei ya mahindi kuzidi kupanda, sasa inakwaje hii? Maana yake bei ya sembe itafanana na kilo ya nyama siku si nyingi...miundo mbinu imeharibika hasa barabara na madaraja, nyumba zinaanguka, wafanya biashara hali ndio imekuwa tete kwelikweli....mvua hii itatuacha na njaa.