barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,863
Mwanzoni mimi niliamini Tanzania nzima hii mwizi ni Edward Lowassa,Toka "kashfa" ya Richmond mwaka 2008 sikuwa nataka kabisa kusikia jina la Edward Lowassa masikioni mwangu.Yaani nilikuwa nikiona tu umeme umekatika namtukania Lowassa kimoyomoyo,mpaka mtaani kwetu mtu ambaye tuliona ana hela "zisizoeleweka" tulimwiita Lowassa au Mzee wa Richmond
Ilikuwa ngumu kunambia kuwa Lowassa ni mtu salama,nilishangaa sana baada ya kujiuzulu akaenda Jerusalem kuhiji akiwa yeye na familia yake kwa maana ya mkewe.Nikajuwa kweli jamaa hatarudi maana kule wanasema wale wenye "madhambi" ya waziwazi huwa hawarudi.Lakini jamaa akarudi na wakampokea kwa nguvu tu wapambe wake baada ya kurudi.
Kila kitu cha wizi nilichokuwa nakisikia nilijuwa Bro Eddo yupo nyuma yake.Aliitwa fisadi papa,mwizi na bingwa wa rushwa.Hata alipotoka hadharani kusema walio na ushahidi waende mahakamani hakuna aliyeenda.Akatoka na kusema kwenye Richmond kila alichofanya hakuna ambacho Mwenyekiti wake alikuwa hajui.Lakini bado hiyo haikuwa sababu ya kumsafisha,ulipokuwa ukitaja ufisadi wa nchi hii basi mimi nilikuwa najuwa ni Eddo tu
Miaka inazidi kwenda,kama naanza kubadili mawazo,kwamba hata kama ni huo ukwapuaji wa kimfumo basi huyu Edward Lowassa sio mwizi kiasi hicho,kuna wengine wakubwa tu,sababu ya kutokuwa na nafasi za kisiasa basi hatukuweza kuwafahamu.Edward sababu ya uanasiasa wake ikawa rahisi kumfahamu,lakini pia nia yake kuelekea kugombea urais ndio ilisababisha kila wizi atupiwe.
Kumbe huyu baba ni kama alibebeshwa mzigo wa wezi wengine.Nilifikiri baada ya Edward kujiuzulu Uwaziri Mkuu,kuondoka CCM na kuja Chadema basi ufaisadi utakuwa umekwisha au kupungua maana tuliambiwa kila wizi wa nchi hii basi Eddo anahusika.Ukisikia umeme umekatika wanasema Bro Eddo,unga ukipanda bei wanasema Eddo,DAWASCO wakikata maji wanasema Eddo,mikopo ikichelewa wanasema ni sababu ya "ufisadi" wa Eddo.Huyu Bro Eddo ni injinia wa kila kitu??
Miaka karibu kumi baada ya Eddo kuipisha serikali kama kiranja mkuu habari ni ile ile.Watu wamepiga bilioni 30+ za mashine za Finger print tena ndani ya Jeshi la Ulinzi na Usalama,yaani tamka kwa nguvu "ULINZI NA USALAMA".Jana Rais Mpendwa JPM akiwa TAZARA katuambia jinsi kampuni ya Simon Group ya Kisena iliyotaka kujibebesha mradi wa DART wenye thamani ya mkopo wa bilioni 336(Tamka kwa nguvu BILIONI 336).Uliza huyu Simoni Kisena ni nani??Uliza rafiki wa karibu wa kawaida na wa kibiashara wa huyu Simon Group ni nani?Jiulize huyu Simoni Kisena toka kuwa mmiliki wa Ginneries za Magu,Mgombea jimbo la Maswa Mashariki mwaka 2010 kupitia CCM hasi kuwa mmiliki wa UDA na baadae "kujimilikisha DART" kuna nani nyuma yake??Na mradi huu wa DART umesimamishwa na pesa za mkopo watakaolipa Watanzania wote lakini kuna watu wanaotaka kujimilikisha wao binafsi wakiwa ni wa familia moja au mbili.TAMISEMI watu walikuwa wanakula mshahara wa marehemu,walioacha kazi na wafanyakazi hewa zaidi ya mamilioni.Huko NIDA tuliambiwa pesa imepigwa na vitambulisho havijakamilika.
Mhasibu huko Singida alikuwa anakula mshiko wa wafanyakazi hewa kila mwezi,yaani kwa mwezi mmoja tu anakula karibu milioni 25 ya wafanyakazi ambao hawapo.Lakini hawa wote ndio walikuwa wanatuambia Tanzania hii "mwizi na fisadi" mkuu ni brother Eddo.Wapo walioshutumiwa kuwatumia dada zao ili kufanya udalali wa kuwaunganisha watu na Rais,hawa ndio walizunguka nchi nzima kusema FISADI nchi hii ni Edward peke yake.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.Huyu mzee tulimtukana sana,yaani ndio akawa nembo ya "ufisadi" nchi nzima,sikuwahi kuwa shabiki wake,lkn wakati unavyozidi kwenda naanza kupata picha kuwa huyu baba ni mvumilivu sana.Kila tusi na kashfa alibebeshwa...Matusi ya kuwa ni mgonjwa wa kujsaidia hadharani,matusi yaliyotukanwa na watoto na vijana ambao ni kama watoto wake.Hakujibu wala kukasirika
Mimi nimejifunza kitu kwa "fisadi" Eddo,uvumilivu na kuacha wakati uongee.Ipo siku ukweli utajulikana nani hasa ni fisadi nchi hii.Kanisa Katoliki liliwahi kumuhukumu Mwanasayansi Galileo Galilei kwa kwenda kinyume na mafundisho yao,lkn miaka zaidi ya 1000 baadae wakaja kugundua wao Kanisa ndio walikosea.Huyu mzee ana mapungufu yake,lakini kuna wengi ametwishwa na kutukanwa.JPM kasaidia kufahamu kuwa kumbe Lowassa pekee sio nembo ya ufisadi wa nchi hii.Kuna hao kina wa bilioni 34 za finger print,kuna wale wa mishahara hewa na bado wale wa mifuko ya Kijamii
Ama hakika wakati ni mwalimu mzuri.Bro Eddo tulikutukana sana Mzee,yaani hakuna tusi hujawahi tukanwa kuanzia 2008 baada ya Richmond...kama ni matusi basi we mzee utakuwa na rekodi ya Guiness Book of Records