Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Walikuwa wanaanza kuzionyesha kuanzia saa tisa mchana huboreki yani CTN ilikuwa moto sana enzi hizo mkuu


Kweli kabisa Mkuu! Na taarifa za habari za CTN mara nyingi alikuwa anatangaza huyu Ephrahim Kibonde. Enzi hizo alikuwa kijana mdogo hata kwa umbo!
 
Daah mkuu unakumbuka hadi mpangilio wa vipindi aisee upo juu sana mkuu yaani wangeweza wangetupatia hata marudio ya vipindi vyoteee
 
Kuna ule mchezo i mean tamthiliya ya kibuyu sijui kama kuna anaeikumbuka aiseee nilikua naogopa si mchezo nilikua naangalia huku nimeziba macho kwa mikono halafu nachungulia
Walikuwa wanarusha channel gani kibuyu
 
nilikua napenda kutazama sana kipindi cha mgongano wa mawazo wale wanafunzi wa sekondari nilikua nawatamania sana na kumuomba mungu siku moja na mi nifike sekondari kama wako teh teh
Kwani saizi hakipo tena
 

Dah! enzi hizo aisee.... Ilikuwa murua sana kukaa mbele ya Luninga.

Sio sasa hivi, ukikaa kwa Luninga kila baada ya dakika mbili tunaona nyimbo za 'akina Diamond Platnumz.
Umeona eee nowadays hakuna kituu kabosa
 
Sijawahi kutazama telenovela za ukweli kama Camila na La muje de Lorenzo,tangu hapo sijaangalia tena,kwa matangazo la jambo lotion lilitisha...na wewe je? Mimi naitwa jambo doogoo
Je unalikumbuka tangazo la seven up la fidodido lilikuwa poa pia
 
Nakumbuka ITV walipozindua tu wakaanza na World Cup 1994 USA. nilikuwa nakesha sitting room peke yangu hadi alfajiri, wakati huo nikiwa kidato cha nne.
kaka utakuwa unakaribia kustaafu.....hahaaha....mi nilivyo hv najiona mzee na kipindi hiko ndo kwaanza nipo la tatu.....wakati ITV inaanza kuna kifaa kilikuwa lazima ununue kiwekwe kwenye TV ili uangalie mpira.....kulikuwa na jamaa mmoja wa kipemba nadhani alikuwa akiitwa Abdi saleh ktk kipindi cha muziki.
 
Kipindi hicho tulikua tunakariri nyimbo zotw za matangazo kama sigara Sm sigara sweetmenthol ni maarufu tanzania yoteee nimesahau maneno,taifa letu tanzania,gazeti letu tanzania mnakumbuka?revolaaa aaa revolaaaa,ule wimbo w chai jaba pia
Sanaaa tulikuwa tunakumbuka sana tuu
 
Wow mi pia revola ndio maana hata id yangu nimeiweka hovyo coz hadi Leo natamani IPP media warudie aisee yule Dada alikuwa na sauti nyororo sn
 
Halafu nilikua napenda kipindu cha the africa journal cha Itv kila j2 yaan kilikua kzur sanaa
Nchi yetu weee niinchi yutuuuuu duuu long long sn kila jumamosi kama sikosei
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…