Tukumbushane hizi hoja zimeishaje?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukumbushane hizi hoja zimeishaje?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tutafika, Feb 3, 2012.

 1. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,385
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 160
  Naomba tukumbushane matukio, hoja na vioja vilivyotokea ambavyo haijulikani hitimisho ilikua ni nini. Hii itatusaidia watanzania kuachana na kasumba ya kwenda na upepo ili tuweze kufikia suluhu katika matatizo yanayotukabili kama nchi.

  Kwa kuanzia:

  1. HOJA YA UFISADI TANROADS:

  Katika hili, aliekuwa anaiongoza hii taasisi ndugu Mrema alisemwa sana, alitukanwa sana, alidharirishwa sana na alifedheheshwa sana (kasoro tu hakuachia ngazi). Baada ya huyu jamaa kumaliza mkataba wake simsikii tena kana kwamba hakuna baya alilo lifanya. Sasa je, alisingiziwa au ni kweli?,

  2. HOJA YA UFISADI WA MNADHIMU JWTZ:

  Huyu nae ilianza kushuka mvua ya tuhuma kwamba kachukua hela nyingi sana za taifa hili na kwenda kuzificha Afrika ya kusini. Hii hoja iliahirishwa (invisible anahusika), je imefikia wapi?

  3. TUKIO LA MAUAJI YA NDUGU MWAIKUSA (Mhadhili wa chuo kikuu cha dar es salaam)

  Mengi yalisemwa hapa kwamba Rais Kagame anahusika, na polis waliahidi kufanyia kazi haraka. Hili tukio kwa mara ya mwisho taarifa nilio nayo ni kwamba wauaji walikamatwa lakini hakuna aliekuwa tayari kusema ni kina nani hao. Je mahakamani watafikishwa lini na kwa sasa wapo gereza gani?

  4. TUKIO LA KULETWA ALSHABAB KUMUUA MWAKYEMBE

  Hili ni kati ya mambo ambayo yalitolewa ushahidi wa kina na mwakyembe mwenyewe polisi, wamefikia wapi?, achilia mbali hili la sasa la kupewa sumu ambalo wanasema hawawezi kuchunguza kwa sababu hawana ushahidi

  5. TUHUMA ZA UFISADI KWA BWANA ROSTAM

  Hivi tuhuma juu ya huyu bwana ni wivu unasumbua maskini wa tanzania au ni kweli? Naona baada ya kuwaachia ubunge wenu mambo sasa ni shwari kabisa!

  6. MADAWA YA KULEVYA

  Hili nadhani ni sugu na halisemeki vizuri tangia enzi hizo. Ngoja mi niongelee mawili tu, kwanza ni tukio la kubambikiwa kesi bwana Reginard Mengi na mtoto wake. Hili aliweka wazi wahusika tena kwa majina na vyeo, sijui liliishaje. Pili ni madawa yaliyokamatwa kule mbeya halafu baadae polisi wakayaiba, imekuwaje hapo? na je madawa ambaya yanakamatwa kila mara yanaenda wapi? na watuhumiwa mbona hatuwaoni mahakamani?. yaani hata kesi moja ya madawa ya lulevya siisikii kabisa!

  7.......................,
   
 2. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,495
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Yaah nikweli mkuu mi nataka kujua tu kuhusu kifo mwaikusa . Nani alihusika.
   
 3. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,365
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  We are buyers of events.
   
 4. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,385
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 160
  Asante, kwenye mantiki huna masahihisho? vip hukumbuki chochote jinsi hayo matukio yalivyoisha?
   
 5. Hagga

  Hagga Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiona kimya jua kuna mkono wa wakubwa hapo
   
 6. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,199
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  si hayo tu hata Oct. 2006 JK kusema atataja majina ya vigogo 50 wa madawa ya kelevya mpaka leo kimyaaa.hii ndiyo Tanzania usanii na danganya watanzania ndiyo order of the day
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,906
  Likes Received: 6,517
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka hilo la namba 4. Kwanza Dr Mwakyembe alidai anatishiwa uhai tukaambiwa uchunguzi unaendelea.
  Akapata ajali Iringa ambayo ilileta kizaazaa kwa wakubwa wa polisi kipingana na taairfia nyingine.
  Mwakyembe akamwandikia IGP na kutaja wahusika wa mpango wa kummaliza. Aliweka magari wamiliki na walioandaliwa kukamilisha mpango huo akiwemo askari polisi, polisi haikusema lolote.
  Sasa Dr anadai kalishwa sumu, anaambiwa upelekwe ushahidi. Ushahidi wa tishio la morogoro kana kwamba haukuwepo.

  Hili ndilo linaendelea na hakika Dr anakila sababu ya kuamini kuwa mikono ni mingi na mingine ni mikubwa.
   
 8. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,716
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  kama la Shimbo waweza kupewa kifungo ndani ya JF
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 10,413
  Likes Received: 2,660
  Trophy Points: 280
  kwani haujajua tabia zetu watanzania??
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,792
  Likes Received: 1,581
  Trophy Points: 280
  Mkuu hizo hoja hazijibiki!

  Nakuongezea moja?: Hatima ya Babu wa Samunge na utafiti wa dawa zake kama zinatibu magonjwa sugu uliishia wapi?
   
Loading...